• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
Mkoa wa Morogoro
Mkoa wa Morogoro

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Morogoro

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Maelezo ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Sehemu na Vitengo
      • Utawala na Rasilimali
      • Serikali za Mitaa
      • Uhasibu na Fedha
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Sheria
      • TEHAMA
      • Afya
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Kitengo cha Habari na Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Morogoro
    • Mvomero
    • Gairo
    • Kilosa
    • Kilombero
    • Ulanga
    • Malinyi
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Morogoro
    • Morogoro DC
    • Mvomero
    • Gairo
    • Ulanga
    • Malinyi
    • Mlimba
    • Ifakara Mji
    • Kilosa
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uchimbaji wa Madini
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
    • Huduma za Ugavi
  • Machapisho
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
    • Fomu Mbalimbali
    • Ripoti mbalimbali
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Videos
    • Hotuba
    • Picha

MWENYEKITI WA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE, APONGEZA UBUNIFU WA MKOA WA MOROGORO.

Posted on: February 17th, 2025


Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara,  kilimo na Mifugo  Mhe. Deo Mwanyika (MB) ameupongeza uongozi wa Mkoa wa Morogoro chini ya Mkuu wa Mkoa huo Adam Kighoma Malima kwa kuja na ubunifu wa kampeni ya "Jisomeshe na Mkarafuu" ambayo itaenda kuinua kipato cha wanafunzi na kuweza kupata mahitaji yao ya msingi ikiwemo Elimu. 


Mhe. Mwanyika ametoa pongezi hizo wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo ya JISOMESHE NA MKARAFUU iliyozinduliwa katika Kata ya Mkuyuni Mkoani humo kwa kuwapatia wanafunzi 800 wa kidato cha kwanza miche 10 kila mmoja ili iweze  kuwasaidia wanafunzi hao katika maisha yao ya baadae hususan katika safari yao ya Elimu kwa kulima zao hilo la karafuu. 


Mhe. Mwanyika amesema, Serikali ya Mkoa wa Morogoro kupitia Mkuu wa Mkoa huo Mhe. Adam Malima imechukua maono ya Mhe. Rais na Wizara ya kuhakikisha na kutekeleza agenda ya kilimo ifikapo 2030, pia kuhakikisha bei elekezi ya mazao ya viungo yanasimamiwa ipasavyo ili kuwainua wananchi kiuchumi. 


"Nakupongeza sana Mhe. Mkuu wa Mkoa huu ni ubunifu mkubwa na mimi niseme tu ukweli hapo nitaiga" amesema Mhe. Deo Mwanyika. 


Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima amesema kuna umuhimu wa kuongeza elimu ya ugani kwa wazazi ili kuondokana na changamoto ya kufa kwa baadhi ya miche ya karafuu huku akitoa ahadi kwa Mhe. Rais kuwa ndani ya miaka mitano  Mkoa wa Morogoro utakuwa eneo la uzalishaji namba mbili wa karafuu duniani. 


Naye Katibu Tawala wa Mkoa huo Dkt. Mussa Ali Mussa akielezea umuhimu wa kampeni hiyo amesema kampeni hiyo inalenga wanafunzi wa kidato cha kwanza  kupanda miche hiyo ili kuwasaidia wanafunzi hao kujisomesha wenyewe kupitia zao la karafuu kwa kuuza karafuu hivyo pia  kukuza uchumi wa familia zao,  Mkoa na Taifa kwa ujumla na ututunzaji wa mazingira. 


Naye Pascal Petro Gabriel mwanafunzi wa kidato cha kwanza shule ya Sekondari ya Mkuyuni amesema wameipokea kwa moyo mmoja kampeni hiyo na kwamba miche hiyo itawasaidia kipindi cha masomo na hata baada ya masomo. 


Baada ya uzinduzi wa Kampeni ya JISOMESHE NA MKARAFUU katika kata ya Mkuyuni Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro Kamati ya Bunge ya Viwanda Biashara kilimo na Mifugo imeendelea na ziara yake ya kukagua shughuli za kilimo katika Kata ya Tawa, ziara hiyo inaendelea Februari 18, 2025 katika Wilaya ya Kilosa na Kilombero. 


MWISHO.

Matangazo

  • MATOKEO YA DARASA LA SABA 2024 October 30, 2024
  • TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI. May 13, 2025
  • View All

Habari Mpya

  • MAFUNZO YA AMIS NA TAUSI YATOLEWA MKOANI MOROGORO.

    May 21, 2025
  • MAFUNZO YA AMIS NA TAUSI YATOLEWA MKOANI MOROGORO.

    May 21, 2025
  • Zaidi ya Mil. 125 zachangwa kupitia chakula cha hisani kukarabati Hospitali ya Rufaa Morogoro.

    May 18, 2025
  • RC MALIMA ASHIRIKI MATEMBEZI YA HISANI, ASEMA HOSPITALI YA RUFAA INAHIMILI WAGONJWA.

    May 17, 2025
  • View All

Video

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima akikagua ujenzi wa jengo la ofisi mpya ya Mkuu wa Mkoa.
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Maelezo ya Mkoa
  • Tangazo la Zabuni
  • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
  • Hotuba
  • Taarifa kwa Umma

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Tanzania
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • TAMISEMI
  • Ikulu
  • Katibu Mkuu Kiongozi
  • Tovuti ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro

    Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO

    Simu: +2550232934305

    Simu: +255766828252

    Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.