Naibu Waziri wa Maji Mhe. Mhandisi Maryprisca Mahundi amekemea vitendo vya baadhi ya viongozi wa siasa kuwatetea wananchi ambao wanafanya shughuli za kibinadamu katika vyanzo vya maji na kusababisha uharibifu wa vyanzo hivyo.
Mhandisi Mahundi ameyasema hayo Oktoba 12 mwaka huu wakati wa kikao na Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge inayoshughulikia maji na mazingira kilichofanyika ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro.
Naibu Waziri huyo amebainisha kuwa vyanzo vya maji vinavyosimamiwa na Bodi ya maji Bonde la Wami/Ruvu hususan vya Mkoani Morogoro vimekuwa vikiharibiwa na shughuli za kibinadamu huku baadhi ya wanasiasa wakiwatetea wananchi hao.
“...vyanzo vya maji vinavyosimamiwa na Wami/Ruvu vimekuwa na changamoto hususan hapa Morogoro wananchi kuingia na kufanya shughuli za kibinadamu na kumekuwa na ugumu kidogo kwa sababu wanasiasa pia wamekuwa wakiingilia...ukienda hapo mindu utamkuta diwani anakujakusimama anatetea lakini ukiangalia anachokitetea ni uharibifu...” amesema Naibu Waziri.
Kamati hiyo ipo Mkoani Morogoro kwa ziara ya siku tatu ambapo itatembelea miradi ya maji ikiwemo Bwawa la Mindu, na Bwawa la Kidunda liliopo Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro.
MWISHO..
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro
Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO
Simu: +2550232934305
Simu: +255766828252
Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz
Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.