• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
Mkoa wa Morogoro
Mkoa wa Morogoro

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Morogoro

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Maelezo ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Sehemu na Vitengo
      • Utawala na Rasilimali
      • Serikali za Mitaa
      • Uhasibu na Fedha
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Sheria
      • TEHAMA
      • Afya
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Kitengo cha Habari na Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Morogoro
    • Mvomero
    • Gairo
    • Kilosa
    • Kilombero
    • Ulanga
    • Malinyi
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Morogoro
    • Morogoro DC
    • Mvomero
    • Gairo
    • Ulanga
    • Malinyi
    • Mlimba
    • Ifakara Mji
    • Kilosa
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uchimbaji wa Madini
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
    • Huduma za Ugavi
  • Machapisho
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
    • Fomu Mbalimbali
    • Ripoti mbalimbali
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Videos
    • Hotuba
    • Picha

PIC YAAHIDI KWENDA KUISHAURI SERIKALI.

Posted on: January 12th, 2025



Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji na Mitaji ya Umma (PIC) imesema, inakwenda kuishauri Serikali kuiwezesha Wakala wa Mbegu Tanzania (ASA) kuwa na Maghala makubwa ya kuhifadhia Mbegu na Mitambo ya kisasa ya kuzalishia mbegu ili kuongeza kasi ya kuzalisha Mbegu za mazao ili kuwa tosherevu kwa watanzania.

Hayo yamebainishwa Januari 12, 2025 na Mwenyekiti wa PIC Mhe. Augustine Vuma (MB) wakati wa ziara ya kamati hiyo Mkoani Morogoro ilipotembelea Makao Makuu ya ASA na kujionea hali halisi ya uhitaji wa maghala ya kuhifadhia mbegu zinazozalishwa.

Mhe. Augustine Vuma amesema, kwa sasa ASA wanazalisha 5% tu ya mbegu za mazao zinazopatikana sokoni ukilinganisha na uhitaji wa watanzania hivyo kufanya sehemu ya asilimia kubwa ya uzalishaji huo kutoka nje ya nchi.

”…lakini jambo la pili lazima Serikali ihakikishe kwamba ASA wanapata Mitambo Mizuri na ya kisasa ili aweze kuzalisha mbegu kwa kasi kubwa zaidi,..” amesema Mwenyekiti huyo.

Kuhusu Kiwanda cha mafuta cha MOPROCO cha Mkoani humo ambacho hakifanyi kazi kwa sasa, amesema ni wajibu wao pia kama Kamati kuishauri serikali kuhakikisha inatafuta namna nzuri ya kumaliza sintofahamu iliyopo baina ya aliyekuwa mwekezaji na Serikali kwa kuwa uwekezaji uliofanyika katika kiwanda hicho ni mkubwa hivyo, kuacha majengo yaliyopo sasa bila kutumika ni kuiletea Serikali hasara.

Kwa upande wake Mbunge wa jimbo la Igunga Mhe. Nicholaus Ngassa  ambaye pia ni mjumbe wa Kamati ya PIC ameipongeza Wizara ya Kilimo chini ya Mhe. Hussein Bashe Waziri wa Kilimo (MB) kwa kusimamia ASA, TARI na TOSCI kufanya kazi kwa ushirikiano hivyo kutimiza ndoto za Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania za kutaka kuwaletea wananchi Maendeleo yao.

Awali,  akimkaribisha Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Mussa Ali Mussa kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa huo Mhe. Adam Kighoma Malima amesema Mkoa  una dhamira ya kulima mazao Matano ya kimkakati  likiwemo zao la Parachichi, Kakao, Mchikichi, Kahawa na mkazo mkubwa upo kwenye zao la Karafuu ambapo hadi sasa Mkoa unazalisha zaidi ya tani 2000 za Karafuu kwa mwaka.

Naye  Mkurugenzi wa Maendeleo ya Mazao kutoka Wizara ya Kilimo Bw. Nyasebwa Chimagu pamoja na kuishukuru Kamati hiyo kwa kutembelea Makao Makuu ya ASA, amebainisha malengo ya Serikali inayoongozwa na Mhe. Dkt.  Samia Suluhu Hassan ya kuhifadhi tani milioni tatu za mazao ifikapo mwaka 2030 ili muda wote serikali iwe na uhakika wa chakula kwa wananchi wake.


MWISHO

Matangazo

  • MATOKEO YA DARASA LA SABA 2024 October 30, 2024
  • View All

Habari Mpya

  • RC MALIMA AKEMEA ULANGUZI WA MAZAO.

    May 08, 2025
  • WAAJIRI MOROGORO WATAKIWA KUTATUA CHANGAMOTO ZA WAFANYA KAZI WAO.

    May 01, 2025
  • SERIKALI KUJENGA BARABARA YA LUPILO – MALINYI KWA KIWANGO CHA LAMI, Bil. 18 ZATOLEWA KUJENGA MADARAJA MAWILI.

    April 25, 2025
  • MWENGE WA UHURU 2025 WATAJA TUNU NNE ZA TAIFA.

    April 19, 2025
  • View All

Video

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima akikagua ujenzi wa jengo la ofisi mpya ya Mkuu wa Mkoa.
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Maelezo ya Mkoa
  • Tangazo la Zabuni
  • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
  • Hotuba
  • Taarifa kwa Umma

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Tanzania
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • TAMISEMI
  • Ikulu
  • Katibu Mkuu Kiongozi
  • Tovuti ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro

    Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO

    Simu: +2550232934305

    Simu: +255766828252

    Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.