Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema Serikali itatoa ushirikiano wa kutosha katika kukamilisha ujenzi wa kiwanda kipya cha Serengeti Sigarate Company limited ambacho kitapunguza changamoto ya ajira kwa vijana hapa nchini.
Dkt. Samia amesema hayo Agosti 6, 2024 wakati wa kuweka jiwe la msingi kiwanda hicha cha sigara kilichopo Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro.
Mhe. Rais amesema kiwanda cha Mkwawa leaf kimesaidia kupunguza uhaba wa ajira kwa vijana, ambapo kimezalisha zaidi ya ajira 7000 na pindi kiwanda cha Serengeti Cigarate company cha sigara kitakapokamilika kitazalisha ajira 12000.
"..nawahakikishie ushirikiano mkubwa katika kujenga kiwanda hiki.." amesisitiza Dkt. Samia
Aidha Dkt. Samia ameagiza viongozi wa Serikali kusimamia wakulima wa zao la tumbaku ili kuwatia moyo wakulima hayo na kuongeza uzajishaji huju akiutaka uongozi wa kiwanda hicho kuunga mkono kwenye kampeni ya nishati safi ya kupikia kwa lengo la kutunza mazingira kwa maendeleo ya Taifa.
Katika hatua nyingine Dkt. Samia ameitaka taasisi hiyo binafsi kuunga mkono programu ya bima ya Afya kwa wote ambayo itaenda kuwasaidia waajiriwa wa kiwanda hicho kupata huduma za afya kwa urahisi kupitia bima hiyo pindi watakapopata matatizo ya kiafya.
Kwa upande wake Mkuu wa mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma malima amesema zao la tumbaku ni miongoni mwa mazao ya kimkakati katika Mkoa huo hasa katika Wilaya za Gairo na Kilosa, hivyo kupitia uzalishaji wa zao hilo unaenda kuongeza upatikanaji wa malighafi hiyo kwa ajili ya kulisha kiwanda hicho.
MWISHO.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro
Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO
Simu: +2550232934305
Simu: +255766828252
Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz
Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.