Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro Mhandisi Emmanuel Kalobelo ameipongeza Halmashauri ya Mlimba Wilayani Kilombero kwa kufanya Kazi kwa ubunifu huku akiitaka Halmashauri hiyo kutumia busara zaidi katika utendaji wao wa kazi.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro Mhandisi Emmanuel Kalobelo (aliyesimama) akitoa ushauri wa kitaalamu wakati wa kikao hicho.
Mhandisi Kalobelo ametoa pongezi na nasaha hizo Mei 12 mwaka huu wakati wa kikao cha Kamati iliyoboreshwa ya Fedha, Uongozi na Mipango ya Halmashauri ya Mlimba Wilayani Kilombero iliyokaa kwa dharura kwa lengo la kuboresha utendaji kazi wa Halmashauri hiyo.
Amesema, kwa uzoefu wa kufanya Kazi Serikalini na kwa muda mfupi aliokuwepo Mkoani Morogoro, ameona Halmashauri ya Mlimba inafanya kazi kwa ubunifu zaidi ukilinganisha na Halmashauri nyingine za Mkoa huo ukiachilia mbali migogoro midogo inayojitokeza ndani ya Halmashauri hiyo.
“sitaki ni pre empty lakini katika halmashauri zilizopo hapa Mkoani kwangu bado ninaona Mlimba inaongoza kwa ubunifu” alisema Mhandisi Kalobelo.
Aidha, amezishauri Kamati mbalimbali za Baraza la Halmashauri hiyo kuwa wanapofika mahali ambapo wanatakiwa kutoa maamuzi makubwa ni lazima wafikirie kwa undani matokeo ya maamuzi hayo yanavyoweza kuathiri Maendeleo ya Halmashauri yenyewe na wananchi wake.
Baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya ya Kilombero wakiwa wanafuatailia kikao hicho. (kushoto ni Katibu Tawala wa Wilaya ya Kilombero Adam Bibangamba)
Sambamba na ushauri huo Katibu Tawala huyo amesema ili Halmashauri yoyote iweze kufanya kazi ILIYOTUKUKA inapaswa kutekeleza mambo matatu muhimu ambayo ni UTAWALA BORA, UWAZI NA USHIRIKISHWAJI, mambo ambayo amesisitiza Baraza la Madiwani na Watendaji wa Halmashauri hiyo kuzingatia na kuyafanyia kazi.
Baadhi ya wataalamu wa Halmashauri ya Mlimba Wilayani Kilombero
MWISHO
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro
Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO
Simu: +2550232934305
Simu: +255766828252
Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz
Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.