Katibu Tawala wa MKoa wa Morogoro Dkt. Mussa Ally Mussa ameishauri Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) kufanya kazi zao kwa Ufanisi, ubora na kumaliza kazi hizo ili kuondoa wasiwasi uliokuwepo kuhusu utendaji kazi wao na kwa kufanya hivyo watatoa Imani kwa Serikali na wadau wengine katika kusimamia ujenzi wa majengo.
Dkt. Mussa Ally Mussa ametoa kauli hiyo leo Machi 20, 2023 Ofisini kwake wakati akisaini Mkataba wa ujenzi wa Jengo la Ikulu Ndogo unaotarajiwa kuanza kujengwa Wilayani Malinyi.
Dkt. Mussa Ally Mussa akiwa anasini mkataba wa ujenzi
Akifafanua zaidi mara baada ya kusaini mkataba huo, Dkt. Mussa amesema anatamani TBA ifanye kazi nzuri na kuondoa makando kando ambayo yalitaka kutokea siku za nyuma na kwamba sasa ijikite katika kufanya kazi yenye ubora, uaminifu na kuzikamilisha kazi hizo kama mkataba unavyoeleza.
“...Ofisi yangu inachokitegemea ni kwamba hii kazi inatafanyika vizuri, kwa ubora unaotakiwa.....” amesema Dkt. Mussa.
Kwa upande wake Meneja wa TBA Kanda ya Morogoro Mhandisi Rebeca Kimambo, pamoja na kutoa shukrani kwa kuiamini TBA na kupata zabuni hiyo, amemhakikishia Katibu Tawala huyo kuwa TBA itafanya kazi iliyosaini kwa ubora unaotakiwa na kukamilisha ujenzi wake kwa wakati.
“...tunaahidi kazi hii tutaifanya kwa weledi na kwa kasi ili mradi uweze kukamilika kwa wakati na kwa ubora unaotakiwa...” amesema Mhandisi Rebeca Kimambo.
Mradi huo ambao ujenzi wake unatarajiwa kuanza mwishoni mwa mwezi Machi mwaka huu utakagharimu zaidi ya Shilingi Milioni 618 na unatarajiwa kukamilika mwezi machi mwaka 2024.Hadi sasa sasa Serikali imekwishatoa shilingi million 500 kwa ajili ya ujenzi huo.
MWISHO
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro
Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO
Simu: +2550232934305
Simu: +255766828252
Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz
Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.