• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
Mkoa wa Morogoro
Mkoa wa Morogoro

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Morogoro

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Maelezo ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Sehemu na Vitengo
      • Utawala na Rasilimali
      • Serikali za Mitaa
      • Uhasibu na Fedha
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Sheria
      • TEHAMA
      • Afya
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Kitengo cha Habari na Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Morogoro
    • Mvomero
    • Gairo
    • Kilosa
    • Kilombero
    • Ulanga
    • Malinyi
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Morogoro
    • Morogoro DC
    • Mvomero
    • Gairo
    • Ulanga
    • Malinyi
    • Mlimba
    • Ifakara Mji
    • Kilosa
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uchimbaji wa Madini
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
    • Huduma za Ugavi
  • Machapisho
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
    • Fomu Mbalimbali
    • Ripoti mbalimbali
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Videos
    • Hotuba
    • Picha

RAS Morogoro awataka Wahandisi Halmashauri kufanya kazi kwa weredi na kujiepusha na vitendo vya rushwa.

Posted on: December 7th, 2023

Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Mussa Ali Musa amewataka Wahandisi wa majengo kufanya kazi kwa weredi ili kuikamilisha miradi kwa wakati uliopangwa huku akiwataka kujiepusha na vitendo vya rushwa.


Ameyasema hayo katika kikao cha pamoja cha majumuisho ya miradi ya ujenzi kilichofanyika katika Halmashauri ya Kilosa Disemba 7, 2023 na kujumuisha Halmashauri zote za mkoa wa Morogoro lengo likiwa ni kujenga uelewa wa pamoja na pia kujifunza teknolojia mpya zinazojitokeza kwenye sekta ya ujenzi.

Ameongeza kuwa baadhi ya Wahandisi hawafiki kuikagua miradi mara kwa mara huku wengine hawatoi ushirikiano wa kutosha kwa wale wanaosimamia na wanaotekeleza miradi hiyo wakiwemo mafundi na kuwataka waandae mipango kazi ili kurahisisha kazi zao.

Aidha amewashauri Wahandisi kuhakikisha wanajenga hifadhi za maji katika miradi mipya hususani kwenye shule hasa za bweni ili zirahisishe uzimaji wa moto endapo likitokea janga la moto kwenye majengo hayo.

Katika kuzijibu changamoto wanazokumbana nazo Wahandisi hao katika kutekeleza majukumu yao, amezitaka mamlaka za kiutawala kuwapa ushirikiano Wahandisi hao huku akiwataka Wahandisi kuwa wabunifu katika kazi zao.

Kwa upande wake Mhandisi Mkuu wa Mkoa Mhandisi Ezron Kilamhama ambaye ndiye muandaaji wa kikao hicho, amesema kuwa lengo la kikao hicho ni kutambua hatua zilizofikiwa katika miradi mbalimbali kwa Halmashauri zote za Mkoa lakini pia kubadilishana uzoefu baina ya Wahandisi wote na kuongeza kuwa utaratibu huu hufanyika kila mwaka ambapo huchaguliwa Halmashauri mojawapo ya kufanyia kikao hicho.

Wakiwasilisha taarifa zao za miradi ya ujenzi, Wahandisi wa Halmashauri zote wamebaisha kuwa ipo miradi iliyokamilika na ambayo haijakamilika na ile iliyoko katika hatua za mwisho huku wakibainisha changamoto wanazokumbana nazo katika utekelezaji wa miradi hiyo.

Naye Mhandisi wa Manispaa ya Morogoro Juma M. Gwiso amesema kuwa miradi mbalimbali imetekelezwa katika Manispaa hiyo ikiwemo ujenzi wa shule ya sekondari kata ya Boma, ujenzi wa soko la wamachinga, ujenzi wa hospitali ya Wilaya, ujenzi wa mabweni ya shule ya sekondari Kilakala, ujenzi wa bwalo la chakula Fungafunga, ujenzi wa kituo cha afya kata ya Tungi, ujenzi wa madaraka manner shule ya sekondari Morogoro na ujenzi wa barabara zenye urefu wa kilometa 12.85

Muwasilishaji kutoka katika Halmashauri ya wilaya ya Morogoro Vijijini ambaye pia ni Kaimu Mkuu wa Divisheni ya Miundombinu wa Halmashauri hiyo Juma Chimwaga amesema kuwa Halmashauri ilipokea shilingi bilioni 8.9 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo huku miradi kadhaa ikiwa imefikia asilimia 90 ya ujenzi. Amesema kuwa zipo changamoto kama vile ukosefu wa usafiri na upungufu wa wataalamu wa ujenzi jambo linalopelekea kuchelewa kukamilika kwa baadhi ya miradi.

Halmashauri nyingine zilizopata nafasi za kuwasilisha  utekelezaji wa miradi ya ujenzi ni pamoja na Halmashauri ya Mji wa Ifakara, Halmashauri ya Ulanga, Halmashauri ya Kilosa, Halmashauri ya Mlimba, Halmashauri ya Mvomero, Halmashauri ya Gairo na Halmashauri ya Malinyi.


MWISHO.

Matangazo

  • MATOKEO YA DARASA LA SABA 2024 October 30, 2024
  • View All

Habari Mpya

  • RC MALIMA AKEMEA ULANGUZI WA MAZAO.

    May 08, 2025
  • WAAJIRI MOROGORO WATAKIWA KUTATUA CHANGAMOTO ZA WAFANYA KAZI WAO.

    May 01, 2025
  • SERIKALI KUJENGA BARABARA YA LUPILO – MALINYI KWA KIWANGO CHA LAMI, Bil. 18 ZATOLEWA KUJENGA MADARAJA MAWILI.

    April 25, 2025
  • MWENGE WA UHURU 2025 WATAJA TUNU NNE ZA TAIFA.

    April 19, 2025
  • View All

Video

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima akikagua ujenzi wa jengo la ofisi mpya ya Mkuu wa Mkoa.
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Maelezo ya Mkoa
  • Tangazo la Zabuni
  • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
  • Hotuba
  • Taarifa kwa Umma

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Tanzania
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • TAMISEMI
  • Ikulu
  • Katibu Mkuu Kiongozi
  • Tovuti ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro

    Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO

    Simu: +2550232934305

    Simu: +255766828252

    Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.