Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Mussa Ali Mussa amewataka wakulima kutunza na kuendeleza teknolojia walizojifunza na kuzitumia katika maeneo yao kwa ajili ya maslahi mapana kwa jamii na Taifa Zima.
Dkt. Mussa amesema hayo Julai 29, 2023 wakati wa hafla ndogo ya mavuno katika kijiji cha Mtego wa Simba kwa kushirikiana na Chuo kikuu cha kilimo cha China ikiwa na lengo la kusherehekea mafanikio ya mradi wa kilimo cha soya.
akifafanua zaidi Dkt. Mussa amesema Jamii inapaswa kutambua mchango wa Chuo hicho katika sekta ya kilimo na kuwataka wakulima Kutumia rasilimali zilizopo yakiwemo maeneo yao madogo kupata mazao mengi kulingana na teknolojia walizojifunza.
"...kwa hii teknolojia mliojifunza mnatakiwa kuitunza na kuendeleza kwa manufaa yenu kwa kutumia rasilimali zilizopo..." amesema Dkt. Mussa Ali Mussa.
Sambamba na hilo, Dkt. Mussa amesema mradi wa soya una mafunzo makubwa sana na inatakiwa kuendeleza kwa ajili ya kupata manufaa zaidi katika jamii zetu.
katika hatua nyingine, Katibu Tawala huyo amesema Mkoa wa Morogoro ni Mkoa tajiri katika mazao mengi likiwemo zao la ndizi kwani migomba ni mali kuliko ndizi ambayo hutengeza nyuzi ngumu kufuma mikoba, mikeka, mazulia na pedi za kike.
Kwa upande wake, Prof. Tang Lixia wa Chuo Kikuu cha Kilimo cha China amesema wana mpango wa kuanzisha mradi wa lishe ya soya shule za Kijiji hicho kwani watoto ni nguvu kazi ya Taifa la kesho, hivyo kukabiliana na tatizo la lishe ni muhimu kwa jamii na Taifa Zima.
Naye, Dkt. Rozalia Rwegasira Katibu Tawala msaidizi sehemu ya uchumi na uzalishaji Mkoa wa Morogoro amesema mradi huo umekuwa na Maendeleo makubwa hasa katika kuwapatia kipato na kujikwamua kiuchumi.
mwisho.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro
Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO
Simu: +2550232934305
Simu: +255766828252
Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz
Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.