Watendaji wa afua tano za Afya, fursa za ujifunzaji wa awali, Ulinzi na usalama wa mtoto na malezi yenye mwitikio wametakiwa kushirikiana katika kutekeleza program Jumuishi ya Taifa ya Malezi, makuzi na maendeleo ya awali ya mtoto ( PJT - MMMAM) ili kufikia malengo ya kuhakikisha malezi na makuzi mazuri kwa watoto yanafikiwa.
Wito huo umetolewa Februari 28, 2025 na Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Mussa Ali Mussa wakati akifungua kikao cha tathimini ya utekelezaji wa program jumuishi ya Taifa ya Malezi, makuzi na maendeleo ya awali ya mtoto ( PJT - MMMAM) kilichofanyika ukumbi wa hospital ya rufaa ya Mkoa wa morogoro.
Dkt. Mussa amesema, kuna umuhimu mkubwa wa watendaji hao wanashirikiana katika kuhakikisha wanatekeleza program zinazoanzishwa zinafanikiwa kwa kuzifikia jamii lengwa ili kufikia malengo ya progrmu hizo zinazoazishwa na Serikali kwa manufaa ya wananchi
"..Hatuna Cordination, mwalimu anafanya kivyake, daktari kivyake, ustawi wa jamii kivyake, kila mtu kivyake mwisho wa siku tunatengeneza program hatuwezi kuzikamilisha .." amesema Dkt. Mussa Ali Mussa.
Kwa upande wake Afisa Ustawi wa Jamii Mkoa wa Morogoro Bi. Jesca Kagunila amesema, katika kutekeleza programu ya PJT - MMMAM, kwa mwaka 2024 MKoa umeweza kufanikiwa kutambua na kusajili vituo vya kulelea watoto (day care center) 357 ambapo vituo vilivyosajiliwa ni 95 sawa na asilimia 27% na vituo visivyosajiliwa ni 262 saw na asilimia 73%.
Pia kama Mkoa umeendelea kutumia vyombo vya habari katika kutoa elimu na kuhamasisha wazazi na walezi kuhusu malezi, makuzi na maendeleo ya mtoto.
MWISHO.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro
Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO
Simu: +2550232934305
Simu: +255766828252
Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz
Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.