Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro Mhandisi Emmanuel Kalobelo ameipongeza Bodi ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanazania – TPA kwa kuongeza ufanisi wa huduma za Bandari hapa Nchini na kuifanya TPA kuwa miongoni mwa mashirika ya Serikali yanayoongoza kwa kutoa gawio kwa Serikali.
Mhandisi Kalobelo ametoa pongezi hizo Novemba 23 mwaka huu akifungua michezo ya Bandari iliyoanza kufanyika katikaUwanja wa Jamhuri ulioko katika Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro Mkoani humo na kushirikisha bandari zote za hapa nchini.
“Pia, napenda kutumia fursa hii kuipongeza Bodi ya TPA na Mkurunzi Mkuu wa TPA Mhandisi Deusdedit Kakoko pamoja na wafanyakazi wote kwa kuongeza ufanisi wa huduma za Bandari na kulifanya shirika letu kuwa moja ya mashirika ya Serikali yanayoongoza katika kutoa gawio kwa Serikali, hongereni sana” amepongeza Mhandisi Kalobelo.
Aidha, Mhandisi Kalobelo amesema, michezo hiyo kwa Mkoa wa Morogoro ni moja ya chachu katika Uchumi kwa kuwa uwepo wake unaongeza mzunguko wa fedha ndaniya Mkoa hususan kwa wafanyabiashara wa Morogoro wakiwemo wenye hoteli, nyumba za wageni na wasafirishaji.
Akiwa karibisha wanamichezo na viongozi wao Mhandisi Kalobelo amewataka kutembelea maeneo ya Utatlii yaliyopo katika Mkoa wa Morogoro ikiwemo mbuga ya wanyama ya Mikumi, Udzungwa, na hifadhi yaTaifa ya Mwalimu Nyerere ambayo sehemu kubwa ya hifadhi hiyo ipo katika Mkoa wa Morogoro.
Katika hatua nyingine Mhandisi Kalobelo amewataka wanamichezo kutoka katika Shirika hilo kufanya michezo hiyo kwa lengo la kutunza Afya na kushinda na kwa nidhamu lakini mara watakaporejea katika sehemu zao za kazi waende kufanya kazi kwa ufanisi, umakini na uadilifu wa hali ya juu.
Hata hivyo, amewakumbusha Wanamichezo hao kuwa ugonjwa wa UKIMWI bado upo hapa nchini hivyo amewataka kuendelea kuwa makini ndani ya mkusanyiko huo na kujikita katika michezo pekee lakini bila kufanya michezo na Afya zao.
Kwa upande wake Bi. Jayne Nyimbo kwa niaba ya Bodi ya Wakurugenzi wa TPA ameweka bayana kuwa Bandari ya Dar es Salaam na bandari nyingine zinaendelea kufanya kazi vizuri na ziko salama katika kuwahudumia wateja wake huku akiupongeza Mkoa wa Morogoro kwa kuwa na mchango mkubwa katika kusafirisha mizigo ya kutoka bandari ya Dar es Salaam kwenda nchi jirani.
Mkurugenzi Mkuu wa TPA Tanzania Mhandisi Deusdedit Kakoko ametaja malengo ya michezo hiyo kuwa ni pamoja na kubadilishana uzoefu katika kazi zao, kujenga umoja miongoni mwao na kujenga Afya za wafanyakazi wao ili wakirudi katika mazingira ya kazi wafanye kazi zao kwa ufanisi zaidi.
Michezo ya Bandari (Interports Games) kwa mwaka huu wa 2020 ni michezo ya 14 na inashirikisha Bandari za Dar es Salaam, Tanga, Mtwara, Bandar iJumuishi ya bandari zote za maji baridi yaani Bandari ya Maziwa na Shirika la Meli la Zanzibar.
Kwa Mkoa wa Morogoro michezo hii imefanyika kwa mara ya tatu mfululizo huku ikihusisha michezo ya mpira wa miguu, kuvuata kamba kwa , kucheza bao na mingine mingi ambapo kwa mwaka jana Bandari ya Dar es Salaam ilibuka kidedea kama mshindi wa jumla kw amichezo yote.
MWISHO
Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.