Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima amesema endapo changamoto kubwa zilizopo Wilayani Ulanga za miundombinu ya Barabara na upatikanaji wa uhakika wa Umeme ndani ya Wilaya hiyo zitaondolewa, Wilaya hiyo inakwenda kufunguka na kukua kiuchumi kwa na kwa mtu mmoja mmoja.
Mhe. Adamu Malima ametoa kauli hiyo Mei 25 mwaka huu wakati anaongea na watumishi wa Serikali wa Wilaya ya Ulanga pamoja na viongozi wa chama wakati wa ziara yake ya kujitambulisha ikiwa ni siku yake ya pili aliyoiaza Mei 24 mwaka huu Wilayani Gairo.
"naenda kuwa msemaji Mkuu wa Ulanga kwanza mkiondoa vikwazo mtaifungua Wilaya hii kupata bilioni 5 Kwa mwaka bila shida yoyote.. ubovu wa barabara za TANROAD gharama zote zitakazotumika kuleta lami Ulanga italipwa na maendeleo ya wananchi naona uzalishaji mkubwa sana..."
amesema Mhe. Adam Kighoma Malima.
Kwa upande mwingine, Mhe. Adam Malima amesema Mkoa wa Morogoro una ardhi ya kutosha kwa ajili ya kilimo hivyo amewataka wataalamu wa Wilaya hiyo kuweka mikakati ya kulinda ardhi hiyo ili kukidhi mahitaji ya wananchi wakizazi cha sasa na vizazi vijavyo Kwa miaka 50 ijayo.
Amesema, ni muhim kwa Viongozi wa Wilaya na Mkoa kuweka mikakati madhubuti ya kulinda rasilimali Ardhi iliyopo katika Wilaya ya Ulanga na Mkoa wa Morogoro kwa jumla kwa kuwa Ardhi ni rasilimali isiyohamishika lakini inayoongezeka thamani Kila inayoitwa Leo.
Katika hatua nyingine Mkuu huyo wa Mkoa amewataka watendaji wote Mkoani humo kuwa makini katika kutoa taarifa za kiutendaji na kuweka takwimu zote zinazohitajika, sahihi na zenye uhalisia kwani hizo ndizo zinazoongoza kupanga mipango ya maendeleo na utoaji wa huduma kwa wananchi kujua huduma zinazohitajika kwa kipindi Gani na na kwamba huduma hizo zielekezwe eneo gani.
Naye Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Mussa Ali Mussa ameshauri watendaji ndani ya Mkoa huo kubadilika kiutendaji na kwenda na Kasi iliyopo sasa kulingana na viongozi waliopo sasa.
Awali akitoa taarifa ya Wilaya ya Ulanga Mkuu wa Wilaya hiyo Dkt. Julius Ningu alibainisha changamoto za Wilaya yake kuwa ni pamoja na Migogoro ya wakulima na Wafugaji changamoto ambayo tayari Mkuu wa Mkoa ameitolea maelekezo kwa Mkuu wa Wilaya na Kamati yake ya Ulinzi na Usalama kuifanyia kazi haraka na kumpa taarifa hatua waliyofikia.
Ziara ya Mhe. Mkuu wa Mkoa Adam Kighoma Ally Malima kesho Mei 26 inaendelea katika Wilaya ya Morogoro.
MWISHO
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro
Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO
Simu: +2550232934305
Simu: +255766828252
Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz
Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.