Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Martine Shigela amempa siku Saba mkuu wa idara ya ardhi wa Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro Patrick Mwakilili kufanya tathmini upya umiliki wa ardhi baina ya Bw. Spilo mwenye Ardhi Eka 500, na Bw. Farid Ally ili kuona kiasi cha ardhi kikichobaki katika Kijiji cha Kiganila Kata ya Selembala katika Halmashauri hiyo.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Martine Shigela akizungumza na wananchi wa Kata ya Selembala Kijiji cha Kiganila wakati wa ziara yake ya kikazi katika Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro ya lukagua miradi ya maendeleo pamoja na kusikiliza na kutatua kero za wananchi.iliyofanyika Juni 23 mwaka huu.
Martine Shigela ametoa agizo hilo Juni 23 mwaka huu wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua miradi ya maendeleo pamoja na kutatua kero mbalimbali zinazowakabili wananchi ambapo pamoja na mambo mengine ameitaka idara hiyo ya ardhi kuwasilisha Ofisini kwa Kiongozi huyo ripoti ya tathmini hiyo kabla au ifikapo Julai mosi mwaka huu.
Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Albart Msando akimkaribisha Mkuu wa Mkoa Martine Shigela ili kuzungumza na wananchi waakati wa ziara ya Mkuu huyo wa Mkoa Juni 23 mwaka huu.
Martine Shigela amesisitiza kwamba migogoro inayojitokeza baina ya wananchi na wawekezaji inatokana na sababu mbalimbali hukuakiwataka wawekezaji kuzingatia kiasi cha ardhi wanachopewa na wananchi na sio kujiongezea ardhi kwa kupora ardhi ya wananchi.
“Niagize idara ya ardhi kufanya tathmini upya kwa kumshirikisha Bw. Farid kuangalia umiliki wa ardhi hiyo kupitia nyaraka zake ili ardhi inayobakia waachiwe wananchi waendelee na utaratibu wao” ameagiza Shigela.
“Lazima tumiliki ardhi kulingana na uhalisia wa nyaraka tulizo nazo na ikifika tarehe mosi Julai naihitaji ripoti ya tathmini hiyo Ofisini kwangu” amesisitiza Shigela.
Katika hatua nyingine Mkuu huyo wa Mkoa amekemea vitendo vinavyofanywa na baadhi ya wafugaji katika maeneo hayo vya kulishia mifugo kwenye mashamba ya wakulima ambapo jambo ambalo lilimkera na kulazimika kutoa agizo la kukamatwa kwa mfugaji mmoja aliyejulikana kwa jina la Mashaka ambaye mifugo yake inashutumiwa kuharibu shamba la mpunga la mkulima mmoja lenye zaidi ya hekari moja.
Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la Polisi ambaye ni Kamanda wa Jeshi hilo Mkoa wa Morogoro Fortunatus Musilimu akiongea na wananchi wa Kata ya Selembala wakati wa ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Juni 23 mwaka huu.
Aidha, Martine Shigela ameitaka Wakala wa Maji Mjini na Vijijini - RUWASA kulipa mifuko 25 ya saruji na DAWASA pia kulipa mifuko 120 ya saruji kwa kusababisha mifuko hiyo kuganda hivyo iletwe mifuko mipya kwa gharama za watendaji wa idara hizo ili shughuli za ukarabati wa visima 8 vya maji uweze kukamilika.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kijiji cha Kiganila Bw. Kondo Maulid amelalamikia baadhi ya askari wa Jeshi la Polisi katika kituo kidogo Polisi tarafa ya Mvuha kutokuwajibika ipasavyo pindi wanapopewa taarifa za uharifu hususa kwa baadhi ya wafugaji kulishia mifugo yao mashamba ya wakulima.
Bw. Kondo ameeleza changamoto ya idara ya Ardhi Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro kutokushughulikia migogoro ya ardhi kijijini hapo kwa wakati hali inapelekea baadhi ya wananchi wa eneo hilo kukosa kufanya shughuli za uzalishaji.
Baadhi ya wananchi wa Kata ya Selembala Kijiji cha Kiganila wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Martine Shigela Juni 23 mwaka wakati ziara katika Kata hiyo.
MWISHO.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro
Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO
Simu: +2550232934305
Simu: +255766828252
Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz
Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.