Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Fatma Mwassa kwenye kikao cha kamati ya ushauri ya mkoa
Mkuu wa wilaya ya kilosa (Mhe. Shaka Hamdu Shaka) akiwa na Mbunge wa kilosa (Pro. Palamagamba Kabudi) kwenye kikao cha kamati ya ushauri ya Mkoa
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Fatma Mwassa amepiga marufuku uuzwaji wa mashamba yaliyorudishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan yaliyopo Mkoani humo yakiwemo mashamba ya Wilaya ya Kilosa huku akimwagiza Mkuu wa Wilaya hiyo Shaka Hamdu Shaka kusimamia agizo hilo la kuacha kuuza mashamba badala yake waweke utaratibu wa kuyagawa mashamba kwa wananchi ili waweze kukuza uchumi wao.
Mhe.Fatma mwassa ametoa agizo hilo machi 7 mwaka huu wakati wa Kikao cha Kamati ya Ushauri cha Mkoa wa katika ukumbi wa Hoteli ya Morena Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro.
“… Mhe. Samia Suluhu Hassan amerudisha mashamba mengi hapa Morogoro jambo la kusikitisha yale mashamba yanauzwa usiku na mchana…naomba kuungwa mkono na iwe sehemu ya maazimio yetu na nitataka kura za wanayoafiki ajenda hii sisi tumesema hatutatoa hati" amesema Fatma Mwassa.
"....Mashamba hayo ni mashamba ya wananchi hasa vijana…” ameongeza Mhe. Fatma Mwassa.
Aidha, Mkuu huyo wa Mkoa amesema mashamba hayo hayatatolewa hati kwa wanunuaji kwani watapewa wananchi wa Morogoro ili kuinua kipato cha wananchi hasa vijana.
Prof. Palamagamba Kabudi Mbunge wa Kilosa akiwa anachangia mada kwenye kikao cha tarehe 7 kamati ya ushauri ya Mkoa.
Kwa upande wake, Mbunge wa Kilosa Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi amepongeza mpango wa matumizi bora ya ardhi ambayo Wakuu wa Wilaya wanatilia mkazo na kusimamia ipasavyo, aidha, ameshauri kuboresha miundombinu ya wafugaji kwa kuwatengea maeneo ya kufugia kwa kufanya hivyo watapunguza au kuondoa kabisa migogoro ya wakulima na wafugaji Mkoani humo.
Mwisho
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro
Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO
Simu: +2550232934305
Simu: +255766828252
Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz
Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.