Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Fatma Abubakar Mwassa amewaapisha Wakuu wa Wilaya za Kilosa na Morogoro walioteuliwa hivi karibuni na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa ajili ya kuongeza kasi ya utendaji kazi katika ngazi hiyo.
Mhe. Shaka Hamdu Shaka Mkuu wa Wilaya ya Kilosa akisaini hati ya kiapo mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Fatm Mwassa.
Mkuu wa Wilaya ya Morogoro (kushoto) Mhe. Rebeca Sanga Nsemwa na Mhe.Shaka Hamdu Shaka Mkuu wa Wilaya ya Kilosa wakila kiapo cha uadilifu leo katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro.
Hafla hiyo ya kuapishwa imefanyika leo Januari 27 katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa huo.
Wakuu wa Wilaya walioapishwa ni Mhe. Shaka Hamdu Shaka ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Kilosa na Mhe. Rebeca Sanga Nsemwa Mkuu wa Wilaya ya Morogoro.
Mara baada ya kuwaapisha, Mkuu huyo wa Mkoa amesisitiza kufanya kazi kwa umoja, kuwa wabunifu, kufanya kazi kwa bidii na kuacha alama za kukumbukwa pindi wamalizapo kuhudumu na kufanya kazi kwa ushirikiano kama timu ili kuyafikia mafanikio na malengo waliojiwekea.
“...sisi ni timu moja, tuache alama”. Amesema Mhe. Fatma Mwassa.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Fatma Mwassa (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na Wakuu wa Wilaya za Morogoro na Kilosa na baadhi ya Wajumbe wa kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa wa Morogoro.
MWISHO.
Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.