Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Malima ametembelea kiwanda kipya cha sukari cha Mkulazi kilichopo Mbigiri Wilayani Kilosa na kuagiza Mkandarasi anayejenga kiwanda hicho kukamilisha ujenzi huo kama walivyokubaliana na hakuna muda wa nyongeza watakaopewa.
Mhe. Adam Malima ametoa agizo hilo Agosti 30, 2023 alipotembelea kiwanda hicho kwa ajiri ya kuangalia hatua iliyofikiwa na maendeleo ya ujenzi wa kiwanda hicho.
Aidha, kutokana na Mkandarasi kusuasua katika kukamilisha wa ujenzi wa kiwanda hicho Mkuu wa Mkoa ametoa siku kumi na nne kuanzia Agosti 30 mwaka huu kukamilisha ujenzi huo na kuruhusu uzalishaji wa sukari kuanza ifikapo septemba 30 mwaka huu.
“...tarehe yetu ya kupokea kiwanda inabaki palepale Septemba 30, 2023 ninyi mkatafute wafanyakazi wa ziada, masaa ya ziada lakini tarehe 30 inabaki palepale hakutakuwa na muda wa ziada...” amesema Mkuu wa Mkoa.
Sambamba na hayo Mkuu wa Mkoa, ametoa wito kwa wakandarasi wanaojenga kiwanda hicho kufika Ofisini kwake na kueleza changamoto zinazokwamisha kukamilisha wa ujenzi wa kiwanda hicho ili ziweze kutatuliwa na kuruhusu kukamilika kwa kiwanda hivyo uzalishaji wa Sukari kuanza.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe Adam Malima akiwaelekeza Jambo wakandarasi wanaojenga kiwanda cha sukari Mkulazi.
MWISHO.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro
Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO
Simu: +2550232934305
Simu: +255766828252
Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz
Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.