RC Malima aagiza TAKUKURU kuchunguza ubadhirifu wa zaidi ya shilingi milioni 400 za vyama vya ushirika.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima amemuagiza Mkuu wa Tasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Wilaya Mvomero kuchunguza ubadhirifu wa fedha shilingi zaidi ya milioni 400 zilizotakiwa kwenda kwa wakulima wa miwa kata ya Mtibwa Wilayani Mvomero kutoka chama cha mikopo cha Turiani (TURISACCOS).
Mhe. Malima ametoa agizo hilo Januari 9 mwaka huu wakati akizungumza kwenye mkutano na vyama vya Ushirika vya wakulima wa miwa Wilayani Mvomero uliofanyika katika ukumbi wa Community Centre uliopo Wilayani humo.
Imeelezwa kuwa kiasi cha zaidi ya shilingi milioni 400 zinadaiwa kuchukuliwa na viongozi hao bila ridhaa ya wakulima hao wa TURISACCOS ambacho kinahudumia wanachama wa vyama vya wakulima wa miwa, kwa sababu hiyo Mhe. Adam Malima amekasirishwa na kitendo hicho na kuagiza Mkuu wa TAKUKURU Wilayani ya Mvomero kushirikiana na Mkuu wa Usalama wa Wilaya hiyo kuchunguza suala hilo ili hatua zaidi zichukuliwe kwa watakaobanika pindi uchunguzi huo utakapokamilika.
Ubadhirifu huo unadaiwa kufanywa na viongozi wa TURISACCOS wakiongozwa na aliyekuwa Mwenyekiti wa chama hicho na viongozi wengine ambapo tayari wamefikishwa mahakamani lakini kesi hiyo inasemekana kufutwa eti kwa sababu ya kukosekana kwa ushahidi.
MWISHO.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro
Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO
Simu: +2550232934305
Simu: +255766828252
Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz
Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.