RC MALIMA AAGIZA WAAJIRI KUUNDA VYAMA VYA WAFANYAKAZI
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima amewaagiza waajiri wote wa sekta ya umma na sekta binafsi kuweka mazingira wezeshi ya kuunda vyama vya wafanyakazi na kuacha kuzoofisha vyama hivyo ndani ya taasisi zao ili kusaidia kutatua changamoto za wafanyakazi na kupunguza migogoro ya kikazi.
Adam Kighoma Malima ametoa Wito huo May 1, 2024 wakati akihutubia siku ya wafanyakazi ambapo kwa Mkoa wa Morogoro maadhimisho hayo yamefanyika Halmashauri ya Mji Ifakara, yakiwa na kaulimbiu isemayo "nyongeza ya mishahara ni msingi wa mafao bora na kinga juu ya hali ngumu ya maisha".
Mkuu huyo wa Mkoa amesema, Serikali ngazi ya Mkoa na Serikali Kuu zitaendelea kushirikiana na viongozi wa vyama vya wafanyakazi kuweka makubaliano ya pamoja ili kuhakikisha vyama hivyo vinawasaidia katika kupata hakim zao na maslai yao kikamilifu.
“……Nitumie fursa hii kwa waajiri wote wa sekta ya umma na sekata binafsi kuwataka kuweka mazingira wezeshi ya kuwepo kwa vyama vya wafanyakazi na kuacha tabia ya kuvizoofisha vyama hivyo kwenye taasisi zenu..” amesema Adam Malima.
Aidha Mhe. Malima ameiagiza ofisi ya Afisa kazi Mkoa na Afya (OSHA) kufuatilia na kufanya ukaguzi wa mara kwa mara ili kujiridhisha kikamilifu mikataba ya wafanyakazi endapo inazingatia sheria na pale penye shida ya mikataba afike haraka na kuishughulikia pia kufanya ukaguzi katika huduma za afya na usalama mahala pa kazi.
Katika hatua nyingine Mhe. Malima amesema kwa mwaka wa fedha 2024/25 Serikali imerejesha utaratibu wa kuwapandisha wafanyakazi madaraja, pia kwa mwaka wa fedha 2022/2023 serikali imetoa ajira mbadala 26514 pia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia SuluhuHassan ametoa kibali cha kuajiri wafanyakazi 46000 katika kibali hicho ajira za walimu ni 12000 na watumishi wa afya ni nzaidi ya elfu 10000.
Kwa upande wake Mratibu wa shirikisho la vyama vya wafanyakazi Mkoa wa Morogoro (TUCTA) Nicholaus Ngowi akisoma taarifa mbele ya Mkuu wa Mkoa ameiomba Seriksali ifanyie kazi maeneo yote ambayo kunamalalamiko ili kuepusha malalamiko yasio ya lazima kwa Wafanyakazi.
Akibainisha kero za wafanya kazi wa Mkoa wa Morogoro amesema kero kubwa ni mishahara duni ambayo haiendani na gharama za maisha, kuchelewesha nyongeza ya misharaha kwa wanafanyakazi wanaopanda madaraja na marupurupu yao na kutolipwa posho kwa wakati.
MWISHO
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro
Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO
Simu: +2550232934305
Simu: +255766828252
Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz
Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.