• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
Mkoa wa Morogoro
Mkoa wa Morogoro

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Morogoro

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Maelezo ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Sehemu na Vitengo
      • Utawala na Rasilimali
      • Serikali za Mitaa
      • Uhasibu na Fedha
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Sheria
      • TEHAMA
      • Afya
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Kitengo cha Habari na Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Morogoro
    • Mvomero
    • Gairo
    • Kilosa
    • Kilombero
    • Ulanga
    • Malinyi
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Morogoro
    • Morogoro DC
    • Mvomero
    • Gairo
    • Ulanga
    • Malinyi
    • Mlimba
    • Ifakara Mji
    • Kilosa
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uchimbaji wa Madini
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
    • Huduma za Ugavi
  • Machapisho
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
    • Fomu Mbalimbali
    • Ripoti mbalimbali
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Videos
    • Hotuba
    • Picha

RC MALIMA AENDELEA KUPAMBANA KUTATUA KERO YA MAJI MANISPAA YA MOROGORO.

Posted on: June 21st, 2025



Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Mhe. Adam Kighoma Malima, ameendelea na juhudi za kutafuta njia mbadala ya kupata maji safi na salama kwa ajili ya wananchi wa mkoa huo akianza na halmashauri ya Manispaa ya Morogoro ambayo maji imekuwa ni kero kubwa na ya muda mrefu kwa wananchi wa Manispaa hiyo.

Mhe. Adam Malima hivi karibuni aliunda kamati iliyoshirikisha wajumbe kutoka taasisi mbalimbali ikiwemo Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Morogoro (MORUWASA), Bodi ya Bonde la Wami - Ruvu, Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) pamoja wa wajumbe kutoka Ofisi yake lengo likiwa ni kutafuta njia mbadala ya kumaliza kero ya maji katika halmashauri ya Morogoro ikiwemo uchimbaji wa visima.

Mnamo  Juni 20, 2025, maono na juhudi hizo za Mkuu wa Mkoa zilianza kuzaa matunda baada ya kutembelea na kukagua zoezi la kuflashi maji kwenye  kisima kimoja wapo chenye urefu wa mita 120, kinachoweza kuzalisha maji lita elfu 40 kwa saa na kitahudumia wananchi zaidi 100,000 kati ya wananchi 250,000 wenye shida ya maji ndani ya Halmashauri hiyo.

Akizungumza baada ya kujionea mwenyewe upatikanaji wa maji hayo, Mkuu wa Mkoa Adam Malima amewataka wananchi wa eneo la Mafisa yalipogundulika maji hayo kuyaachia maeneo yao na kutoa ushirikiano wa kutosha katika kufanikisha azma hiyo ya kupata maji kwa faida ya jamii nzima huku Serikali ikiendelea na uratibu wa kuwatafutia fidia ya nyumba na viwanja vyao.

"...Siwezi kuacha mtu analima mahindi hapa halafu Mafisa nzima haina maji, na mimi naweza kuchimba maji. Nikasema, mimi ndiye Mkuu wa Mkoa; lawama zote nitazibeba mimi. Chimbeni maji," amesisitiza Mhe. Adam Malima.

Aidha, Mkuu huyo wa Mkoa amewaagiza wataalamu kujenga tanki la maji katika eneo hilo la Mafisa ili kuhudumia wakazi wa eneo la Mafisa, Kayenzi, na maeneo ya jirani, huku akitoa rai kwa wananchi kutunza chanzo hicho cha maji na miundombinu yake itakayojengwa eneo hilo. 

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa MORUWASA, CPA Sais Kyejo, ameahidi kuendeleza ushirikiano na kuhakikisha mradi huo unakamilika kwa mafanikio, pamoja na kuahidi kutekeleza maelekezo ya Mkuu wa Mkoa huku akiwahakikishia wananchi kuwa Mradi huo unalenga kuongeza vyanzo vya maji na kuboresha huduma ya maji kwa wakazi wa Manispaa ya Morogoro.

Naye Katibu Tawala Msaidizi, Sehemu ya Miundombinu Mkoa wa Morogoro, Mhandisi Ezron Kilamhama, amesema uchimbaji wa kisima hicho katika eneo hilo unaonyesha uwezekano wa kuchimba visima vingine viwili, na hivyo kufanya jumla ya visima vitatu jambo ambalo litapunguza kwa kiasi kikubwa changamoto ya upatikanaji wa maji katik manispaa hiyo.


MWISHO.

Matangazo

  • MATOKEO YA DARASA LA SABA 2024 October 30, 2024
  • TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI. May 13, 2025
  • View All

Habari Mpya

  • RC MALIMA AENDELEA KUPAMBANA KUTATUA KERO YA MAJI MANISPAA YA MOROGORO.

    June 21, 2025
  • WAHARIRI NCHINI WAPATIWA MAFUNZO USIMAMIZI WA MNYORORO WA UGAVI.

    June 17, 2025
  • ZAIDI YA TRILIONI 3 ZATEKELEZA MIRADI YA MAENDELEO MKOANI MOROGORO

    June 16, 2025
  • UPUNGUFU WATUMISHI WAIBUKA HOJA ZA CAG MLIMBA.

    June 11, 2025
  • View All

Video

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima akikagua ujenzi wa jengo la ofisi mpya ya Mkuu wa Mkoa.
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Maelezo ya Mkoa
  • Tangazo la Zabuni
  • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
  • Hotuba
  • Taarifa kwa Umma

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Tanzania
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • TAMISEMI
  • Ikulu
  • Katibu Mkuu Kiongozi
  • Tovuti ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro

    Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO

    Simu: +2550232934305

    Simu: +255766828252

    Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.