Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima amefurahishwa idadi ya watu wengi waliojitokeza kujiandikisha katika daftari la wapiga kura huku akihimiza waendelee kujitokeza ili waweze kujiandikisha na kushiriki uchaguzi wa Serikali za mitaaa uliopangwa kufanyika Novemba 27, 2024.
Mkuu wa Mkoa Adam Malima amesema hayo leo Oktoba 11, 2024 wakati akishiriki zoezi la kujiandikisha katika daftari la wapiga kura katika kituo cha Lita kilichopo Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro ikiwa ni siku ya kwanza kati ya siku kumi zilizotengwa kwa ajili ya wwnanchi kushiriki zoezi hilo la kujiandikisha.
Aidha, amesema kituo hicho kinatarajia kuandikisha watu 506 ambapo kwa siku ya leo pekee watu 200 wamejitokeza kujiandikisha hivyo amekiri kufurahishwa kwake na mwitikio wa watu waliofika kujiandikisha na kwamba hiyo ni alama tosha kuwa wananchi wanajua umuhimu wa kujiandikisha kwa maendeleo ya Taifa.
"..nitumie fursa hii kuwashukuru sana maana nyie mmekuwa mfano kwa Morogoro nzima kwa kujitokeza kwa wingi katika zoezi hili la uandikishaji .. " amesema Mhe. Adam Malima
Sambamba na hayo amewataka watu waliojitokeza katika zoezi hilo kuwa mabalozi wazuri kwa wenzao na kwamba uandikishaji ni wajibu wa kila mtanzania ili aweze kushiriki uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa maendelao yao na Taifa la Tanzania.
MWISHO.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro
Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO
Simu: +2550232934305
Simu: +255766828252
Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz
Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.