Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima amefurahishwa na ziara ya Maafisa elimu na walimu Wakuu kutoka visiwani Zanzibar ziara iliyolenga kupata uzoefu katika nyanja mbalimbali za elimu ikiwemo usimamizi wa miradi ya elimu, taaluma pamoja na kudumisha muungano wa Zanzibar na Tanganyika.
Mhe. Malima ameyasema hayo Februari 10 mwaka huu wakati wa kikao cha majumuisho ya ziara ya Maafisa Elimu hao kilichofanyi kakatika ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa huo.
Mkuu huyo wa Mkoa amesema kwake ni faraja kuona miaka 60 ya Mapinduzi walimu kutoka Zanzibar wanafika kufanya ziara ya mafunzo Mkoani humo na kubainisha kuwa Walimu hao wameongeza kitu kwa walimu wa Mkoa huo.
"...na leo miaka 60 ya Mapinduzi kuona walimu mmekuja kama hivi kwa kujitolea na kufanya ziara ya mafunzo kwangu mimi ni fahari kubwa sana yaani nimejisikia faraja sana...nimejifunza jambo kubwa sana..." amesema sisitiza Mkuu huyo wa Mkoa.
Aidha, amesema kuwa nchi hizo mbili zina malengo mbalimbali yanayofanana kwenye sekta ya elimu ikiwemo kuongeza ufaulu wa wanafunzi na kufuta daraja sifuri, kudhibiti utoro na changamoto ya uhaba wa walimu wa masomo ya Sayansi na kusema kuwa Mkoa unaendelea na jitihada za kuhakikisha kuwa malengo hayo yanafikiwa.
Katika hatua nyingine, Mhe. Adam Kighoma Malima amewasisitiza walimu hao kuzingatia masuala ya lishe kwa watoto ili kuondoa hali ya udumavu pia amewataka kusimamia maadili ya watoto na kupiga vita utamaduni wa kigeni ambao unasababisha mmomonyoko wa maadili hapa nchini.
Naye Afisa Elimu Sekondari kutoa Mkoa wa Kusini - Pemba Bw. Seif Mohammed Seif amesema lengo la ziara hiyo ni kujifunza mambo mbalimbali kwenye sekta ya elimu Mkoani humo ikiwemo uboreshaji wa taaluma na usimamizi wa miradi ya elimu huku akiusifu Mkoa wa Morogoro kwa kutekeleza miradi ya elimu kwa fedha za mapato ya ndani na kwamba wamefurahiswa na jambo hilo na wanakwenda kulifanyia kazi.
Aidha, amewapongeza viongozi wa Mkoa wa Morogoro kwa kuweka mikakati mahususi ya kudhibiti nidhamu na utoro shuleni kupitia uhamasishaji wa utoaji wa chakula mashuleni na lishe kwa wanafunzi wake.
MWISHO.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro
Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO
Simu: +2550232934305
Simu: +255766828252
Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz
Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.