Mkuu wa Mkoa wa Morogoro ameutaka uongozi wa Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro kujikita katika utunzaji wa mazingira kwa upandaji wa miti hususan mazao ya biashara yakiwemo karafuu na michikichi katika maeneo ya milimani.
Mhe. Malima ameyasema hayo Februari 5, 2024 wakati wa kikao cha kupitia bajeti ya Halmashauri hiyo kwa mwaka wa fedha 2024/2025 kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa huo.
Mkuu huyo wa Mkoa amebainisha kuwa upandaji wa mazao ya biashara itasaidia kukuza uchumi wa wananchi, Halmashauri na Mkoa kwa ujumla hivyo akautaka uongozi kuhakikisha wanazingatia utunzaji wa mazingira.
“...kwahiyo tunachosema ni kwamba kwenye hii vita ya kuokoa mazingira, ya kupanda miti ‘it must be targeted’ kwenye mambo mawili mazingira na maisha...” amesema Mkuu wa Mkoa.
Aidha, ameitaka Halmashauri hiyo kuwachukulia hatua watakao haribu mazao yatakayopandwa kutokana na umuhim wa mazao hayo kwenye uchumi wa Mkoa wa Morogoro.
Katika hatua nyingine Mhe. Malima ameitaka Halmashauri hiyo kuongeza juhudi katika ukusanyaji wa mapato zaidi matumizi sahihi ya fedha na yasiyo na maswali wakizingatia kuwa halmashauri yao inatakiwa kuwa ni mfano kwa Halmashauri nyingine kwa ndani ya Mkoa huo.
Kwa upande wake Katibu Tawala Mkoa wa Morogoro Dkt. Mussa Ali Mussa ameisisitiza Halmashauri pamoja na kujikita kwenye kilimo cha mazao kama michikichi, kakao, parachichi na karafuu ambayo ni rafiki lakini pia kwa upande wa miti kupanda miti ambayo ni rafiki kwa binadamu moja kwa moja ili asiweze kuikata kwa kuwa ina faida kwake hususan maeneo ya milimani.
MWISHO.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro
Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO
Simu: +2550232934305
Simu: +255766828252
Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz
Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.