• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
Mkoa wa Morogoro
Mkoa wa Morogoro

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Morogoro

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Maelezo ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Sehemu na Vitengo
      • Utawala na Rasilimali
      • Serikali za Mitaa
      • Uhasibu na Fedha
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Sheria
      • TEHAMA
      • Afya
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Kitengo cha Habari na Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Morogoro
    • Mvomero
    • Gairo
    • Kilosa
    • Kilombero
    • Ulanga
    • Malinyi
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Morogoro
    • Morogoro DC
    • Mvomero
    • Gairo
    • Ulanga
    • Malinyi
    • Mlimba
    • Ifakara Mji
    • Kilosa
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uchimbaji wa Madini
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
    • Huduma za Ugavi
  • Machapisho
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
    • Fomu Mbalimbali
    • Ripoti mbalimbali
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Videos
    • Hotuba
    • Picha

RC Malima aridhishwa na utekelezaji wa miundombinu, atoa maagizo

Posted on: October 5th, 2023

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Ali  Malima amesema ameridhishwa na utendaji kazi wa Wakala wa barabara Vijijini na Mijini (TARURA) na  Wakala wa barabara Tanzania (TANROADS) Mkoa wa Morogoro  kwa kazi kubwa na nzuri inayofanywa na Taasisi hizo hususan katika ujenzi wa Madaraja na Barabara huku akitoa maagizo kwa watendaji wa Serikali kutoa Elimu kwa wananchi wa Berega na vijiji jirani kutunza miundombinu hiyo ambayo ndio chachu ya kukuza uchumi na kuisaidia kupata huduma muhimu za Afya, Elimu Maji na usafirishaji.

Mhe. Malima amesema hayo Oktoba 4 mwaka huu wakati wa ziara yake ya kutembelea miradi ya maendeleo.


 Mhe.  Malima  akiambatana na wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa amefanya ziara hiyo katika wilaya za Kilosa na Mvomero kwa lengo la kujionea utekelezaji wa miradi hiyo ya barabara.


Miundombinu aliyotembelea kiongozi huyo ni pamoja na ufukuaji mchanga katika Daraja la Dumila, Karavati zinazojengwa barabara ya Morogoro - Dodoma eneo la Mvomero na ujenzi wa daraja la Berega.


 Miradi mingine ni ujenzi wa karavati yanayojengwa barabara ya Kilosa - Mikumi na Daraja la Luhemba ambako liko Wilayani Kilosa.


 Akiwa Katika mradi wa daraja la Berega ambako ujenzi wake utagharimu shilingi Bil. 7.9 hadi kukamilika kwake, amewaagiza watendaji wa  Wilaya hiyo akiwemo Afisa Tarafa, Mtendaji Kata na watendaji wa Vijiji kuhakikisha wananchi wa Berega na maeneo jirani wanatunza miundombinu ya daraja hilo kwa kuwa ni kiunganishi kikubwa baina ya Mkoa wa Morogoro na Mkoa wa Tanga, lakini pia litasaidia wananchi kufika kwenda Hospitali ya Berega kupata matibabu kipindi chote cha mwaka tofauti na awali ambapo kulikuwa na changamoto hususan kipindi cha masika.


Aidha, amewataka wananchi hao kutofanya shughuli za kijamii kando Kando ya mto wa daraja hilo hususan shughuli za kilimo ili daraja hilo  liweze kudumu kwa muda mrefu.


"...nimefarijika sana na mradi huu katika hatua iliyofikia, kwa hakika tuna kila sababu ya kumshukuru Dkt. Samia Suluhu Hassan kupata Daraja kubwa namna hii...hivyo nawaomba sana wananchi wa vijiji jirani kuacha kulima maeneo yaliyokaribu na miundombinu kama huu kwa ajili ya kulitunza lizidi kubaki imara..." amesema Mhe. Adam Malima.


Aidha, Mkuu huyo wa Mkoa amesema daraja hilo  lina manufaa makubwa ya kiuchumi na kijamii kwa watanzania wote kwa ujumla hivyo hakuna budi kulilinda.


Katika hatua nyingine, Mkuu huyo wa Mkoa akiwa katika Mradi wa ujenzi wa Daraja la Ruhembe Wilayani Kilosa amesema Serikali imetoa fedha kutekeleza miundombinu kwani inategemewa na watanzania katika shughuli za kiuchumi na kijamii na kuwataka Wakandarasi wa mradi huo kutekeleza majukumu yao ipasavyo ili kukamilisha Daraja hilo kwa matumizi ya wananchi.


Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Mhe. Shaka Hamdu Shaka amesema Daraja la Berega litakapokamilika litasaidia kwa sehemu kubwa kwenye usafilishaji wa bidhaa ikiwemo za nafaka kwa kipindi chote cha mwaka hivyo uchumi wa Kilosa utakuwa maradufu.


Nae, Mhandisi Maghesa Khamis , Mkandarasi mzawa katika Mradi wa Daraja la Berega akitoa taarifa ya ujenzi wa mradi huo amesema mradi umefikia 99% ambapo utakamilika Oktoba 8, mwaka huu na Daraja hilo kuanza kutumika rasmi.



Mwisho

Matangazo

  • MATOKEO YA DARASA LA SABA 2024 October 30, 2024
  • View All

Habari Mpya

  • RC MALIMA AKEMEA ULANGUZI WA MAZAO.

    May 08, 2025
  • WAAJIRI MOROGORO WATAKIWA KUTATUA CHANGAMOTO ZA WAFANYA KAZI WAO.

    May 01, 2025
  • SERIKALI KUJENGA BARABARA YA LUPILO – MALINYI KWA KIWANGO CHA LAMI, Bil. 18 ZATOLEWA KUJENGA MADARAJA MAWILI.

    April 25, 2025
  • MWENGE WA UHURU 2025 WATAJA TUNU NNE ZA TAIFA.

    April 19, 2025
  • View All

Video

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima akikagua ujenzi wa jengo la ofisi mpya ya Mkuu wa Mkoa.
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Maelezo ya Mkoa
  • Tangazo la Zabuni
  • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
  • Hotuba
  • Taarifa kwa Umma

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Tanzania
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • TAMISEMI
  • Ikulu
  • Katibu Mkuu Kiongozi
  • Tovuti ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro

    Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO

    Simu: +2550232934305

    Simu: +255766828252

    Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.