Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima ameridhishwa na kasi ya utendaji kazi wa shirika la usafiri wa anga la Tanzania (Air Tanzania) kasi iliyo na bunifu katika kuwahudumia wateja wake hasa Watanzania ambao ndio wateja wanaokusudiwa.
Mhe. Malima amesema hayo aprili 20, Mwaka huu wakati akifunga mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa shirika la usafiri wa anga hapa nchini(Air Tanzania) uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Kings way hotel uliopo Halmashauri ya manispaa ya Morogoro Mkoani Morogoro.
"...tangu serikali ilipowekeza kuongeza vifaa na ndege mpya mwaka 2016 mpaka sasa ni miaka 8 Air Tanzania imebadilika sana na inafanya vizuri sana hongereni Air Tanzania... " amesema Mhe. Adam Malima
Pia, Mhe. Adam amesema Mkoa huo unavivutio vingi vya utalii vikiwemo milima ya uduzungwa, mbuga ya wanyama ya mikumi na Bonde la Akiba la kilombero, hivyo kipaumbele kitakuwa Air Tanzania katika kusafirisha watalii kutokana na huduma zao bora na kuvutia watalii wengi zaidi Mkoani humo.
Sambamba na hilo, Mhe. Malima amewataka Wafanyakazi wa shirika hilo kuwa wawajibikaji, wenye nidhamu na bora zaidi ya sasa kwa manufaa ya Taifa.
Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya ndege Tanzania (ATCL) Mhandisi Ladislaus Matindi amesema kupitia usafiri wa ndege unasaidia fursa mbalimbali zikiwemo za utalii ambazo zinapatikana na kufikika kwa urahisi ndani na nje ya nchi kwa maslahi mapana ya nchi.
Nae, Msimamizi wa kituo cha Air Tanzania nchini Kenya amesema Baraza hilo limejadili mwenendo, malengo sambamba na mipango mikakati waliojiwekea mwaka wa 2023/2024 ili 2024/2025 kuweza kufanya vizuri zaidi.
MWISHO
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro
Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO
Simu: +2550232934305
Simu: +255766828252
Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz
Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.