• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
Mkoa wa Morogoro
Mkoa wa Morogoro

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Morogoro

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Maelezo ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Sehemu na Vitengo
      • Utawala na Rasilimali
      • Serikali za Mitaa
      • Uhasibu na Fedha
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Sheria
      • TEHAMA
      • Afya
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Kitengo cha Habari na Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Morogoro
    • Mvomero
    • Gairo
    • Kilosa
    • Kilombero
    • Ulanga
    • Malinyi
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Morogoro
    • Morogoro DC
    • Mvomero
    • Gairo
    • Ulanga
    • Malinyi
    • Mlimba
    • Ifakara Mji
    • Kilosa
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uchimbaji wa Madini
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
    • Huduma za Ugavi
  • Machapisho
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
    • Fomu Mbalimbali
    • Ripoti mbalimbali
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Videos
    • Hotuba
    • Picha

RC MALIMA ASHIRIKI MATEMBEZI YA HISANI, ASEMA HOSPITALI YA RUFAA INAHIMILI WAGONJWA.

Posted on: May 17th, 2025


Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Alhaji Adam Kighoma Malima amesema Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro inahimili kupokea wagonjwa wengi kwa wakati mmoja kutokana na uwekezaji mkubwa alioufanya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kutoa fedha nyingi kwa ajili ya kuboresha majengo  na kununua vifaa tiba vya kisasa.

Mhe Malima amesema hayo Mei 17, 2025 mara baada ya matembezi ya hisani ya miaka 80 ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa huo yakiambatana na kaulimbiu isemayo "MIAKA 80 YA UJENZI WA JAMII YENYE AFYA " .


Mhe. Malima amesema uwezo wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro umekuwa mkubwa na kuweza kuhimili wagonjwa wengi baada ya Dkt. Samia Suluhu Hassan kutoa takribani Tsh Bilioni 7.8 kwa ajili ya kuboresha majengo yakiwemo Jengo la mama na Mtoto na vifaa vya kisasa kama vile  CT Scan, Digital X-Ray, Mtambo wa kufua hewa tiba ya oksjeni, Kifaa cha uchunguzi wa sikio, koo na pua, mashine zaidi ya kumi za kuchuja damu (Dialysis).

".. Wagonjwa wote wanapata huduma kwa pamoja na hii ni ishara ya Hospitali hii kuhimili mambo makubwa.." amesema Mhe. Malima.

Aidha Mhe. Malima ameupongeza uongozi wa Hospitali hiyo kwa kazi kubwa na nzuri wanayoifanya jambo linalopelekea  kuiheshimisha  hoapitali hiyo na kuwatendea haki wanamorogoro na watanzania wengine kwa kutoa huduma nzuri na kwa wakati.

Katika hatua nyingine Mkuu huyo wa Mkoa amewakumbusha wakazi wa Mkoa huo kushiriki kuboresha taarifa zao katika daftari la kudumu la wapiga kura awamu ya pili ili waweze kupata haki ya kuchaguliwa na kumchagua kiongozi wanayemtaka na ambaye ni bora katika kuwaongoza na kuwasemea.

Kwa upande wake Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Morogoro Dkt. Daniel Nkungu amesema kuanzia Mei 5 hadi 9, 2025 huduma ya afya cheki imefanyika bure, pia upasuaji kwa wale waliogundulika kuhitaji huduma hiyo  ulianza kufanyika kuanzia Mei 12 hadi 16 na kutolewa bure ambapo  jumla ya waliopatiwa huduma hiyo  ni wananchi 3772, wakiwemo 242 waliofanyiwa upasuaji.

Nae Boniventura Mpeka wa kutoka Mvomero kwa niaba ya wananchi wenzake amesema, huduma imayotolewa katika hospitali hiyo ni nzuri na imeboreka kwa ukilinganisha na miaka minne iliyopita, kwa sasa wahudumu wanatoa huduma zao kwa welidi na kutumia vifaa vya kisasa hivyo ameishukuru Serikali kwa kuwaboreshea hospitali hiyo.


MWISHO.

Matangazo

  • MATOKEO YA DARASA LA SABA 2024 October 30, 2024
  • TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI. May 13, 2025
  • View All

Habari Mpya

  • RC MALIMA ASHIRIKI MATEMBEZI YA HISANI, ASEMA HOSPITALI YA RUFAA INAHIMILI WAGONJWA.

    May 17, 2025
  • VYAMA VYA SIASA NCHINI VYATAHADHARISHWA

    May 15, 2025
  • RC MALIMA ATAKA VYAMA VYA USHIRIKA VYA WAFUGAJI

    May 15, 2025
  • Vyama vya Ushirika Vyatakiwa Kutumia TEHAMA

    May 14, 2025
  • View All

Video

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima akikagua ujenzi wa jengo la ofisi mpya ya Mkuu wa Mkoa.
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Maelezo ya Mkoa
  • Tangazo la Zabuni
  • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
  • Hotuba
  • Taarifa kwa Umma

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Tanzania
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • TAMISEMI
  • Ikulu
  • Katibu Mkuu Kiongozi
  • Tovuti ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro

    Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO

    Simu: +2550232934305

    Simu: +255766828252

    Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.