Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam kighoma Ali Malima amewataka wanawake wa Kiislam Mkoa wa Morogoro kuwa na umoja na ushirikiano baina yao katika kukemea na kutokomeza tabia chafu zinazoletwa na kuigwana baadhi ya watanzania na kisha kuharibu jamii.
Mhe. Malima ameitoa kauli hiyo leo Julai 14, 2024 wakati akihutubia Baraza la Wanawake la Waislamu 2023/2024 lililofanyika katika Msikiti wa Bomaroad uliopo Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro.
Kiongozi huyo amesema licha ya uwepo wa uvunjifu wa Mila na desturi za kitanzania bado kuna uwepo wa tabia chafu na zisizofaa ndani ya jamii yetu zikiwemo ndoa za jinsia Moja yaani ushoga na usagaji.
Kwa sababu hiyo Mhe. Adam Kighoma Malima amewataka akinamama hao kuwa na umoja na ushirikiano baina yao kwa sababu wao ni nguzo muhimu katika Jamii katika kufanikisha vita ya kutokomeza vitendo hivyo vichafu katika jamii ya watanzania.
"..Nakuombeni mama zangu, myaangalie haya, mkawe wapiganaji namba Moja kuitetea hii jamii juu ya vitendo viovu..." Amesisitiza Mhe. Malima
Aidha, amewaasa akina mama hao wa kiislamu kuwa na utaratibu wa kuwafuatilia watoto ili kujua mienendo yao na kuepuka watoto hao kuharibika kwa kuiga tabia hizo zisizofaa hususan la kuingiliana kinyume na maumbile wanaume kwa wanaume -Ushoga na Usagaji kwa wanawake.
Katika hatua nyingine amemshuruku Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutoa fedha za asilimia 10 kwa ajili ya mikopo ya vijana,wanawake na makundi maalum na kuwataka akina mama hao wa kiilsamu na akinamama wengine wasio wa kiislam kuchangamkia fursa hiyo na kutengeneza vikundi vyao vya kina mama na kukopa fedha hizo kwa ajili ya kufanya biashara zao ili kujikimu Kimaisha na kuacha kukopa mikopo isiyo na faida na inayoumiza maarufu kama "kusha damu".
Kwa upande wake Katibu wa Baraza la Wanawake la Wailsam Manispaa ya Morogoro Bi. Amina Hussein ameeleza changamoto zinazo kwamisha utekelezaji wa kazi katika baraza lao zikiwemo ukosefu wa compyuta, printer, photocopy mashine, pamoja na mikopo ya kausha damu.
Naye Bi. Mwazani Mussa Mwenyekiti wa wanawake Waislam Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro amesema katika kupambana na matendo mabaya katika jamii wanaendelea kutoa elimu mashuleni na misikitini kwa watoto na wanawake wote ili kuhakikisha vitendo hivyo vinatokomezwa.
Hata hivyo mwenyekiti huyo amewataka wanawake kuwa karibu na familia zao hasa kwa watoto wao ili kujua maendeleo yao lakini pia kutobweteka katika kufanya kazi badala yake wafanye kazi zikiwemo za ujasiriamali ili kuweza kuongeza kipato chao na familia zao kwa ujumla.
MWISH
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro
Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO
Simu: +2550232934305
Simu: +255766828252
Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz
Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.