• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
Mkoa wa Morogoro
Mkoa wa Morogoro

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Morogoro

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Maelezo ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Sehemu na Vitengo
      • Utawala na Rasilimali
      • Serikali za Mitaa
      • Uhasibu na Fedha
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Sheria
      • TEHAMA
      • Afya
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Kitengo cha Habari na Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Morogoro
    • Mvomero
    • Gairo
    • Kilosa
    • Kilombero
    • Ulanga
    • Malinyi
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Morogoro
    • Morogoro DC
    • Mvomero
    • Gairo
    • Ulanga
    • Malinyi
    • Mlimba
    • Ifakara Mji
    • Kilosa
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uchimbaji wa Madini
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
    • Huduma za Ugavi
  • Machapisho
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
    • Fomu Mbalimbali
    • Ripoti mbalimbali
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Videos
    • Hotuba
    • Picha

RC MALIMA ASISITIZA UONGOZI WA HAKI, UWAJIBIKAJI NA USHIRIKIANO

Posted on: January 29th, 2025

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima amemtaka Mkuu wa Wilaya ya Ulanga aliyeteuliwa hivi karibuni Mhe. Khamana Juma Simba kufanya kazi yake kwa haki, uwajibikaji na ushirikiano mkubwa baina yake na viongozi wengine wa serikali wa sekta zote ndani ya Wilaya yake.


Mkuu huyo wa Mkoa ametoa rai hiyo Januari 29, Mwaka huu wakati wa hafla fupi ya uapisho wa Mkuu wa Wilaya huyo iliyofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa huo na kuhudhuriwa na viongozi wa Chama na Serikali.


Mhe. Malima amsema Mkuu huyo wa Wilaya anatakiwa kufanya kazi yake kwa kufuata misingi ya uongozi wa haki, uwajibikaji, ushirikiano na kujituma katika kutekeleza majukumu yake na kufuata misingi ya uongozi ili kuleta amani na utulivu pamoja na maendeleo katika jamii.


“ukienda huko utakutana na kila aina ya watu wakubwa kwa watoto na hutakiwi kuweka ukubwa wako kwanza badala ya kuweka dhamana yako juu yao” amesema Mhe. Adam Malima


Aidha, Mhe. Adam amemtaka Mkuu huyo wa Wilaya ya Ulanga kushughulika kikamilifu  kutatua migogoro ya wakulima na wafugaji inayoikabili Wilaya hiyo kwa kuzingatia maadili ya katiba na sheria za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.


Kwa upande wake, Kaimu Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Morogoro, Bw. Stephen Magoiga amemshauri Mkuu huyo wa Wilaya kufuata yale yote yaliyo kwenye katiba na kanuni za uongozi ili kutekeleza majukumu yake kwa weledi huku akisimamia sheria na uwajibikaji.


Akizungumza baada ya kula kiapo, Mhe. Simba ameahidi kushirikiana na wananchi wa ngazi zote katika kuleta maendeleo ya Wilaya ya Ulanga.


“naomba kuchukua fursa hii kuwaomba watu wa Ulanga, viongozi wezangu wa chama na Serikali, watumishi wa serikali na wananchi wote wa wilaya ya Ulanga tufanye kazi ya kuwasaidia wana Ulanga ya kuwaletea maendeleo, nina amini tukishirikiana pamoja tutafanya vizuri na kuistawisha wilaya yetu ya Ulanga” Amesema Mhe. Simba


Mwisho.

Matangazo

  • MATOKEO YA DARASA LA SABA 2024 October 30, 2024
  • View All

Habari Mpya

  • RC MALIMA AKEMEA ULANGUZI WA MAZAO.

    May 08, 2025
  • WAAJIRI MOROGORO WATAKIWA KUTATUA CHANGAMOTO ZA WAFANYA KAZI WAO.

    May 01, 2025
  • SERIKALI KUJENGA BARABARA YA LUPILO – MALINYI KWA KIWANGO CHA LAMI, Bil. 18 ZATOLEWA KUJENGA MADARAJA MAWILI.

    April 25, 2025
  • MWENGE WA UHURU 2025 WATAJA TUNU NNE ZA TAIFA.

    April 19, 2025
  • View All

Video

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima akikagua ujenzi wa jengo la ofisi mpya ya Mkuu wa Mkoa.
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Maelezo ya Mkoa
  • Tangazo la Zabuni
  • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
  • Hotuba
  • Taarifa kwa Umma

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Tanzania
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • TAMISEMI
  • Ikulu
  • Katibu Mkuu Kiongozi
  • Tovuti ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro

    Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO

    Simu: +2550232934305

    Simu: +255766828252

    Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.