Siku moja baada ya vyombo vya habari kuripoti juu ya watu kadhaa kuangukiwa na matofali katika hospitali ya Platinum iliyopo Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro, Mkuu wa Mkoa huo Mhe. Adam Kighoma Malima ametembelea hospitali hiyo na kuagiza Mhandisi wa Mkoa na timu yake kwenda katika hospitali hiyo ili kujiridhisha ubora wa jengo hilo ndani ya siku mbili kabla hajaruhusu hospitali hiyo kuendelea kutoa huduma kwa wananchi.
Mhe. Malima ametoa kauli hiyo Oktoba 17, mwaka huu baada ya kutembelea hospitalini kujionea hali ya tukio hilo kama ilivyoripotiwa na vyombo mbalimbali vya Habari huku akifafanua kuwa kilichotokea sio ukuta kunguka bali ni matofali machache yaliyokuwa yanatumika katika ujenzi uliokuwa unaendelea kuanguka na kuleta kadhia hiyo ya kujeruhi baadhi ya watu kama ilivyoripotiwa.
”...Hatutaki kuifungia kwa muda mrefu lakini tunataka kuangalia hicho kilichosababisha ajali hiyo jana…maamuzi yangu ni kwamba wataendelea kusimama mpaka Mhandisi wa Mkoa na wenzake watakuja wataangalia hayo marekeb9isho…halafu kwa yale maeneo ambayo yanaweza kutoa huduma basi huduma ziendelee...” amesema Mkuu wa Mkoa.
MWISHO.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro
Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO
Simu: +2550232934305
Simu: +255766828252
Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz
Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.