• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
Mkoa wa Morogoro
Mkoa wa Morogoro

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Morogoro

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Maelezo ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Sehemu na Vitengo
      • Utawala na Rasilimali
      • Serikali za Mitaa
      • Uhasibu na Fedha
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Sheria
      • TEHAMA
      • Afya
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Kitengo cha Habari na Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Morogoro
    • Mvomero
    • Gairo
    • Kilosa
    • Kilombero
    • Ulanga
    • Malinyi
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Morogoro
    • Morogoro DC
    • Mvomero
    • Gairo
    • Ulanga
    • Malinyi
    • Mlimba
    • Ifakara Mji
    • Kilosa
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uchimbaji wa Madini
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
    • Huduma za Ugavi
  • Machapisho
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
    • Fomu Mbalimbali
    • Ripoti mbalimbali
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Videos
    • Hotuba
    • Picha

RC MALIMA AWAONYA WAFUGAJI, WATATHMINI MALI, ATAKA TABIA YA MIFUGO KULA MAZAO YA WAKULIMA IKOME

Posted on: June 10th, 2024

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima amewaonya baadhi ya wafugaji wenye tabia ya kulishia mifugo yao mazao ya wakulima kwa makusudi na kwamba tabia hiyo ikome mara moja badala yake waheshimiane.


Adam Kighoma Malima ametoa agizo hilo Juni 10, 2024 wakati wa ziara yake akiambatana na  Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa huo kufanya ziara ya kukagua miundombinu mbalimbali Mkoani humo itakayofanyika kwa siku tatu.

Akiwa katika Kitongoji cha Mtakenini Wilayani Mvomero kukagua matengenezo ya Barabara ya Doma – Kilosa - Maharaka alipokea kero kutoka kwa wananchi wa kitongoji hicho namna wanavyosumbuliwa na baadhi ya wafugaji kulisha mifugo kwenye mazao yao likiwemo zao la nyanya.

Mhe. Adam Malima amesema, ni vema makundi hayo mawili ya Wafugaji na wakulima yakaheshimiana kwa kuwa kila upande umehiari wenyewe kufanya kazi wanayoifanya, hivyo mkulima amheshimu mfugaji na mfugaji amheshimu mkulima kwani kila mmoja kachagua kazi hiyo kwa hiari yake.

Hata hivyo, amekemea vikali baadhi ya wafugaji wanaoingiza mifugo yao kwa makusudi kwenye mashamba ya wakulima na mifugo yao kula mazao ya wakulima na kwamba huo ni udhalimu wa kiwango cha juu na kuitaka tabia hiyo ikome mara moja.

“nakwambia Mkuu wa Wilaya na wewe Mkurugenzi na Mwenyekiti wa Halmashauri tengenezeni utaratibu ili Mvomero tabia hii ife kabisa na ikome” amesisitiza Mhe. Malima


Amewataka wafugaji kama wanataka kulisha mazao ya wakulima wafanye utaratibu wa kuingia makubaliano na wenye mazao kwa kulipa fedha ili mkulima apate haki yake na mfugaji aweze kulisha mazao hayo kwa uhuru zaidi

Katika hatua nyingine  Mkuu huyo wa Mkoa amewageukia Watathmini Mali wanaokadiria hasara inayotokana na mifugo kula mazao ya wakulima kuacha tabia ya kupokea rushwa kutoka kwa baadhi ya wafugaji na kukadiria hasara hizo chini ya kiwango kinachotarajiwa.

Naye Meneja wa Maji Mijini na Vijijini – RUWASA amemwahidi Mkuu wa Mkoa wa Morogorokukamilisha mradi wa maji unaoendelea kukamilishwa katika eneo hilo mwishoni mwa mwezi huu wa Juni huku Mkuu wa Mkoa akiongeza wiki mbili hivyo Julai 15 kazi ya kuwapelekea wananchi hao maji iwe imekamilika.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kitongoji cha Mtakenini kwa niaba ya wananchi wenzake kero sugu zinazowasumbua  katika eneo lao ni Pamoja na Barabara, Wanyama tembo kuvamia mashamba yao pamoja na uhaba wa maji.

 

MWISHO

Matangazo

  • MATOKEO YA DARASA LA SABA 2024 October 30, 2024
  • View All

Habari Mpya

  • RC MALIMA AKEMEA ULANGUZI WA MAZAO.

    May 08, 2025
  • WAAJIRI MOROGORO WATAKIWA KUTATUA CHANGAMOTO ZA WAFANYA KAZI WAO.

    May 01, 2025
  • SERIKALI KUJENGA BARABARA YA LUPILO – MALINYI KWA KIWANGO CHA LAMI, Bil. 18 ZATOLEWA KUJENGA MADARAJA MAWILI.

    April 25, 2025
  • MWENGE WA UHURU 2025 WATAJA TUNU NNE ZA TAIFA.

    April 19, 2025
  • View All

Video

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima akikagua ujenzi wa jengo la ofisi mpya ya Mkuu wa Mkoa.
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Maelezo ya Mkoa
  • Tangazo la Zabuni
  • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
  • Hotuba
  • Taarifa kwa Umma

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Tanzania
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • TAMISEMI
  • Ikulu
  • Katibu Mkuu Kiongozi
  • Tovuti ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro

    Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO

    Simu: +2550232934305

    Simu: +255766828252

    Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.