Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima amewapongeza Masista wa upendo wa Mtakatifu Fransisko kilichopo Mbingu Wilayani Kilombero Mkoani humo kwa uwekezaji wanaoufanya katika Sekta ya kilimo, ufugaji na kijamii.
Mkuu wa Mkoa Mhe. Adam Malima akimsalimia sista mmojawapo katika kituo cha upendo wa Mtakatifu Fransisko.
Mhe. Malima ametoa pongezi hizo Juni 8 mwaka huu alipotembelea Kituo hicho cha masista kwa lengo la kuwapa pole ya kuvamiwa katika kituo hicho mwanzoni mwa mwezi huu na watu wasiojulikana na kupora baadhi ya mali zao .
Hapa Mhe. Adam Malima ana imba wimbo pamoja na Masista.
Sambamba na pongezi hizo akiwa kituoni hapo Mkuu wa Mkoa amesema kwa uwekezaji wanaoufanya kwenye miradi ya Afya, elimu, maji na umeme wa maji, na kuongeza kasi ya maendeleo yao na jamii inayowazunguka kwa jumla.
Hapa Mkuu wa Mkoa anapokea risala kutoka kwa msomaji wa risala hiyo.
kuhusu mgogoro wa ardhi uliopo baina yao na wananchi wa eneo hilo, Mhe. Adam Malima amemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mlimba Mhandisi Stephen Kaliwa kutuma wataalam wa idara ya ardhi kutoka katika Ofisi yake kwa kushirikiana na viongozi wa kituo hicho kupitia nyaraka zote za umiliki wa eneo hilo ili maamuzi yatakayotolewa yawe ya haki.
"...hili la ardhi DED yupo, DED atakaa na watu wake wa ardhi mtakuja kuangalia lile eneo, muangalie documents zao zinavyosema na kunipa mrejesho..."amesema Mhe. Adam Malima.
Mhe. Adama Malima akizungumza na viongozi pamoja na Masista wa upendo wa Mtakatifu Fransisko baada ya kuwasili kituoni hapo.
aidha, Mkuu huyo wa Mkoa amewashauri Viongozi wa kituo hicho kushirikiana na wadau mbalimbali wa maendeleo wenye nia ya kuwekeza katika nyanja mbalimbali walizowekeza kwa lengo la kuongeza tija zaidi.
Kwa upande wao Masista wa upendo wa Mtakatitu Frasisko wamebainisha changamoto zinazowakabili ikiwemo mgogoro wa ardhi baina ya kituo hicho na wananchi wa Kijiji cha Mbingu, wakibainisha kuwa mgogoro huo unasababishwa na baadhi ya viongozi wa kijiji kuahidi kupitia majukwaa ya kampeni za uchaguzi kuwapatia wananchi sehemu ya ardhi ya kituo hicho, huku wakijua wazi kuwa ardhi hiyo ni mali ya kituo hicho.
changamoto nyingine ni ukosefu wa mawasiliano ya simu hali ambayo hupelekea kutofikisha haraka ujumbe unaokusudiwa na kumwomba Mkuu wa Mkoa kuwasaidia kupata mnara wa mawasiliano jambo ambalo Mkuu wa Mkoa alisema amelipokea na anakwenda kushughulika nalo.
shirika la masista wa Upendo wa Mtakatifu Fransisko lilianzishwa mwaka 1944 huko Mahenge Mkoani Morogoro askofu Mkapuchini kwa lengo kuu la kujitakatifunza.
Lakini pia Shirika hilo linajishughulisha na kuwahudumia watu kiroho na kimwili hususan wale watu walio katika mazingira hatarishi wakiwemo kutunza wazee wasiojiweza au kutelekezwa na ndugu zao,kuwatunza wenye matatizo ya ukoma na ugonjwa wa kifafa, wenye mtindio wa ubongo na yatima.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Malima (wa tatu kushoto walio kaa) akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa chama na serikali na masista wa Upendo wa Mtakatifu Fransisko baada ya kuongea nao.
MWISHO.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro
Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO
Simu: +2550232934305
Simu: +255766828252
Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz
Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.