Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Ali Malima amewataka wahe. Madiwani wa Halmashauri ya Mlimba Wilayani Kilombero Mkoani humo kuwa na wivu wa Maendeleo kwa lengo la kuendeleza Halmashauri hiyo.
Mhe. Adam Malima amesema hayo wakati wa kikao cha Baraza la Madiwani cha kujadili hoja za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kilichofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa halmashauri Mlimba.
Amesema, Wahe. Madiwani hawana budi kuwa na wivu wa kimaendeleo badala ya kuwa Madiwani wasioitakia mema Halmashauri yao na wananchi wake huku akiwakumbusha kuwa Halmashauri hiyo ni yao na kwamba hawana sehemu nyingine ya Kwenda kama ilivyo kwa watendaji wa Serikali wanaohamishwa kila wakati.
“Sasa mimi nachukia nikikuta sina madiwani wenye wivu wa maendeleo wana wivu wa kupiga” amesisitiza Mhe. Malima.
Pamoja na kuwataka waheshimiwa Madiwani kuwa na wivu wa kimaendeleo, amewataka kutekeleza Ilani ya chama chao kivitendo ikiwemo kusimamia mfumo wa stakabadhi ghalani ambao ndio mfumo wenye uhakika kwa mwananchi wao kuuza mazao yao kwa bei ya faida hivyo kujikwamua kiuchumi.
Awali akifungua kikao hicho Mkuu wa Mkoa huyo aliwapongeza wahe. Madiwani hao kwa Halmashauri yao kushika nafasi ya kwanza kati ya Halmashauri tisa za Mkoa huo kwa ukusanyaji wa mapato, usimamiaji wa Miradi ya Maendeleo Pamoja na masuala ya Elimu.
Naye Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo ya Mlimba Mhe. Innocent Mwangasa amelaani uwepo wa viashiria vya majungu vinavyojitokeza katika Halmashauri hiyo na kumuomba Mkuu wa Mkoa na viongozi wengine kuendelea kuwa karibu nao katika kufanya vikao ili kuvikomesha vitendo hivyo.
Halmashauri ya Mlimba imepata hatia safi (hati inayoridhisha) kwa miaka mitano (5) mfululizo na katika kikao cha leo, Baraza chini ya mwenyekiti wake Mhe. Mkuu wa Mkoa mejadili jumla ya hoja sita (6) na zote zimepewa muda wa kuzikamilisha ili hoja hizo zifungwe.
MWISHO
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro
Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO
Simu: +2550232934305
Simu: +255766828252
Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz
Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.