Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Ali Malima amewataka vijana kujiunga kwenye vikundi ili kupata mikopo ya 10% inayotolewa na kila Halmashauri ikiwa ni juhudi ya Serikali kupambana na umasikini.
Mhe. Malima ametoa wito huo Disemba 2, 2023 wakati akifunga bonanza ya vijana iliyoandaliwa kwa lengo la kutoa ajira kwa vijana kupitia pfogram ya SET na OYE bonanza iliyoandaliwa na kudhaminiwa na serikali ya uswizi nia kubwa ikiwa ni kuwajengea uwezo vijana kuwa wajasilia mali katika sekta mbalimbali kama vile ufugaji, uvuvi, kilimo na ufundi stadi.
Aidha, Mhe. Malima amebainisha kuwa fedha za asilimia kumi zipo katika Halmashauri zote za Mkoa wa Morogoro hata hivyo amebainisha kuwa fedha hizo hazitolewi kwa mtu mmoja mmoja bali hutolewa kwenye vikundi ambavyo vimesajiliwa na kukidhi vigenzo.
"...wote wanaosajili vikundi kwa hawa kupitia hela za SET wakafanya vizuri wakahitaji hela ya ziada na kwenye Halmashauri hizo Hela za 10% zipo zinasubiri vijana mjisajili mzipate..." amesema Mkuu wa Mkoa Malima.
Sambamba na hilo, Mkuu huyo wa Mkoa amesisitiza vikundi hivyo kurejesha fedha hizo kwa wakati ili kuuweka mfuko kuwa hai na vijana kuaminiwa na serikali yao katika utekelezaji wa majukumu ya kukuza uchumi wao, Mkoa na Taifa kwa ujumla.
Kwa upande wake, Balozi wa uswizi hapa nchini Bw. Didier Chassot amesema mafunzo hayo ni muhimu sana kwa vijana katika kuwajengea uwezo sambamba na ubunifu ambapo mabanda mbalimbali aliyoyaona yameonesha ubunifu katika kazi zao, hivyo mafunzo hayo yamekuwa muhimu kwa vijana ambao ndio tegemeo la kesho.
Naye, Meneja wa mradi wa Fursa za ajira kwa vijana (OYE) amesema mradi huo unafanya kazi na vijana wote kuanzia miaka 18-35 ambao hawapo katika mfumo wa elimu ukiwa na lengo la kuboresha maisha ya vijana unaojikita zaidi katika upatikanaji wa ajira kwa vijana, kupata ujuzi mbalimbali kwa vijana hao.
Mwisho.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro
Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO
Simu: +2550232934305
Simu: +255766828252
Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz
Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.