Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima amewahimiza viongozi wa dini kutumia nafasi zao na kuhubiri amani na upendo kwa waumini wao kwa lengo la kuwajenga kiimani ili kuweza kuishi kwa kuheshimiana na kustamihiliana.
Mhe. Malima ameyasema hayo leo Oktoba 16, 2024 wakati akiongea na viongozi wa dini wa Wilaya ya Kilombero mkoani Morogoro ikiwa ni ziara yake ya kikazi ya siku mbili Wilayani Ulanga, Malinyi na Kilombero.
Aidha Mhe. Malima amewasisitiza viongozi hao kushiriki katika kujiandikisha katika daftari la wapiga kura ili kukidhi matakwa ya kuchagua na kuchaguliwa katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika Novemba 27, 2024 na kupata viongozi walio na manufaa kwa Jamii na Serikali kwa kipindi cha miaka mitano ijayo.
Pia Mhe. Adam Malima amewashukuru viongozi hao wa dini kwa kushiriki na kufanikisha Ziara ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati wa Ziara yake ya kikazi Mkoani Morogoro.
Kwa upande wao viongozi wadini wamempongeza Mkuu huyo wa Mkoa kwa uongozi ulio tukuka na kumshukuru kwa kutenga muda wa kukutana nao na kumuahidi kuendelea kuliombea Taifa, kutunza amani na kutoa ushirikiano Kwa Serikali katika zoezi la Uchaguzi wa Serikali za Mitaa.
MWISHO.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro
Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO
Simu: +2550232934305
Simu: +255766828252
Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz
Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.