• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
Mkoa wa Morogoro
Mkoa wa Morogoro

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Morogoro

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Maelezo ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Sehemu na Vitengo
      • Utawala na Rasilimali
      • Serikali za Mitaa
      • Uhasibu na Fedha
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Sheria
      • TEHAMA
      • Afya
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Kitengo cha Habari na Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Morogoro
    • Mvomero
    • Gairo
    • Kilosa
    • Kilombero
    • Ulanga
    • Malinyi
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Morogoro
    • Morogoro DC
    • Mvomero
    • Gairo
    • Ulanga
    • Malinyi
    • Mlimba
    • Ifakara Mji
    • Kilosa
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uchimbaji wa Madini
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
    • Huduma za Ugavi
  • Machapisho
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
    • Fomu Mbalimbali
    • Ripoti mbalimbali
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Videos
    • Hotuba
    • Picha

RC Malima awataka Viongozi wa dini kushirikiana na Serikali kupambana na mmomonyoko wa maadili.

Posted on: November 19th, 2023

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Ali Kighoma Malima amewataka viongozi wa dini kuwa mfano katika kupambana na mmomonyoko wa maadili hapa nchini na kuwafundisha vijana kudumisha maadili na tamaduni za kiafrika ili kuwa na kizazi kitakachokuwa na tija katika maendeleo.

Mhe. Malima amesema hayo Novemba 19, 2023 alipohudhuria Baraza la maulidi la Mkoa wa Morogoro lililofanyika kata ya Dakawa Wilayani Mvomero Mkoani humo ambapo alialikwa kuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo. 

Aidha, Mkuu huyo wa Mkoa amesema maadili ya jamii yetu yanaharibiwa na utamaduni wa mataifa ya Maghaharibi kupitia mitandao ya kijamii hususan vijana ambao ndio tegemeo kwani wameanza kubadili jinsia ya kiume kutaka kuwa jinsia ya kike, ya kike kuwa ya kiume na matumizi ya dawa za kulevya sambamba na mienendo isiyofaa ambayo hukwamisha  juhudi za serikali za kufikia malengo iliyojiwekea.

"...kwa hiyo niwasihi ndugu zangu tunatakiwa kuwa mfano katika kupambana na madawa ya kulevya kwa kushirikiana na Serikali ili kulinda kizazi hiki na kijacho..." amesema Mhe. Adam Malima


Katika hatua nyingine, Mhe. Adam Malima amesisitiza Baraza hilo kuhakikisha kuwa na Masheikh waliosoma Elimu ya dini ya kiislam na kuijua vizuri katika kuendeleza vema elimu hiyo kwa vizazi vilivyopo na vijavyo.

Kwa upande wake, Sheikh wa Mkoa wa Morogoro Sheikh Twaha kilango amethibitisha kutoa ushirikiano katika uongozi wake na serikali ili kupunguza baadhi ya majukumu ikiwemo kutoa elimu ya kimaadili kwa wananchi ili kuinusuru jamii ya kitanzania kuathirika na tamaduni zisizofaa.

Naye, Amili wa ujenzi wa misikiti sehemu zisizo na misikiti  Mkoani Morogoro Sheikh Ibrahim Musa Makange amesema mmomonyoko wa maadili ikiwemo utumiaji wa madawa umekithiri hususan kwa vijana ambao ndio tegemeo la Taifa, hivyo amemhakikishia Mkuu wa Mkoa kuendelea kuchukua hatua ili kuleta maendeleo ya Mkoa huo na Taifa kwa ujumla.


Mwisho.


Matangazo

  • MATOKEO YA DARASA LA SABA 2024 October 30, 2024
  • View All

Habari Mpya

  • RC MALIMA AKEMEA ULANGUZI WA MAZAO.

    May 08, 2025
  • WAAJIRI MOROGORO WATAKIWA KUTATUA CHANGAMOTO ZA WAFANYA KAZI WAO.

    May 01, 2025
  • SERIKALI KUJENGA BARABARA YA LUPILO – MALINYI KWA KIWANGO CHA LAMI, Bil. 18 ZATOLEWA KUJENGA MADARAJA MAWILI.

    April 25, 2025
  • MWENGE WA UHURU 2025 WATAJA TUNU NNE ZA TAIFA.

    April 19, 2025
  • View All

Video

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima akikagua ujenzi wa jengo la ofisi mpya ya Mkuu wa Mkoa.
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Maelezo ya Mkoa
  • Tangazo la Zabuni
  • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
  • Hotuba
  • Taarifa kwa Umma

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Tanzania
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • TAMISEMI
  • Ikulu
  • Katibu Mkuu Kiongozi
  • Tovuti ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro

    Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO

    Simu: +2550232934305

    Simu: +255766828252

    Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.