Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima amewataka wananchi wa Mkoa huo kujitokeza kwa wingi kujiandikisha kwenye daftari la wapiga kura, zoezi linalotarajia kuanza kesho Oktoba 11 hadi 20, 2024 na kusisitiza kuwa zoezi hilo ni muhim kwa kila mwananchi ili aweze kushiriki uchaguzi wa Serikali za Mitaaa hapo Novemba 27 mwaka huu.
Mhe Malima ametoa wito huo Oktoba 10, 2024 wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi yake ambapo kwa mwakaa huu uchaguzi wa serikali za mitaaa una kaulimbiu inayosema " Serikali za Mitaa, Sauti ya Wananchi, Jitokeze kushiriki Uchaguzi"
Aidha Mhe. Malima amesema maandalizi ya uandikishaji wa wapiga kura yamekamilika katika Mkoa huo ikiwa ni pamoja na upokeaji wa madaftari ya kuandikisha wapiga kura na kusambazwa katika vituo litakapofanyika zoezi la uandikishaji hivyo amesema ni wajibu kwa kila mwananchi kushiriki kikamilifu katika zoezi hilo la kujiandikisha.
"... Wito wangu ni kwa kila mwananchi mwenye sifa kuanzia miaka 18 na kuendelea kujitokeza kujiandikisha ili kuwa na haki yake ya kupiga kura .." Amesisitiza Mhe. Adam Malima.
Amesema, kupitia sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022 Mkoa wa Morogoro unakadiriwa kuwa na jumla ya wakazi 3,200,000 ambapo kwa mwaka
2024 kupitia vigezo mbalimbali Mkoa huo utakuwa na jumla ya wapiga kura 1,816,500 waliokidhi vigezo vya wapiga kura.
Pia Mkuu huyo wa Mkoa amesema Mkoa huo utakuwa na jumla ya vituo 3,752 ambapo Halmasahuri ya wilaya ya Kilosa ina vituo 814, Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro vituo 734, Morogoro Manispaa vituo 294, Mlimba vituo 265, Ifakara Mji vituo 257, Ulanga vituo 222, Malinyi vituo 163, Mvomero vituo 687 na Gairo vituo 316, huku waandikishaji 3,998 tayari wameshapatiwa mafunzo kwa ajili ya kuanza zoezi hilo.
Sambamba na hayo Mhe. Malima amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa uongozi imara na nia yake ya kuhakikisha kila mtanzania mwenye sifa za kupiga kura anashiriki uchaguzi wa Serikali za Mitaa huku pia akimshukuru kwa kuwafikishia watanzania maendeleo ya kisiasa, Kijamii na Kiuchumi.
MWISHO.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro
Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO
Simu: +2550232934305
Simu: +255766828252
Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz
Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.