Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima ameendelea na ziara yake Wilaya za Kilombro, Malinyi na Ulanga pamoja na mambo mengine ya kusikikiza kero za wananch ziara hiyo ina lengo la kunusuru Pori la akiba la Kilombero kwa kuzuia uharibifu unaoendelea kupitia shughuli za kibinadam ili kuliwezesha bwawa la Mwalimu Nyerere kupata maji ya kutosha.
Akiwa katika kata ya Wilayani Malinyi January 19, 2024 Mhe. Malima ameongea na wananchi waKijiji hicho na kuwapa uelewa wa namna ya kutunza mazingira katika pori hilo ili kuruhusu upatikanaji wa maji ya kujaza maji katika bwawa la Mwalimu Nyerere kwa ajili ya kuzalisha umeme utakaotumika kwa maendeleo ya Tanzania nzima.
“…… hili jambo tunalolifanya hapa ni kwa ajili ya kuinusuru maslai mapana ya Tanzania nzima..” amesema Mhe. Adam Malima.
Pia Mhe. Malima ametembelea mto Mnywela na kujionea adha ambayo wananchi wanakumbana nayo hasa kipindi cha Masika hususa ubovu wa miundombinu kama Barabara, na upungufu wa vivuko vya kuvusha wananchi kutoka upande mmoja hadi upande wa pili.
Hata ivyo amesema katika Kijiji cha Mombwe kuna mifugo mingi sana ambayo inapelekea uharibifu wa mazingira katika mto mnywela hivyo kuna mpango wa kuwahamisha haraka ili kunusuru uharibifu wa mito ya eneo hilo ambayo inapeleka maji katika bwawa la Mwalimu Nyerere kwa ajili ya uzalishaji wa umeme.
Kwa upande wake Kamishana msaidizi mwandamizi Joas Makwati ambae ni kamanda wa hifadhi nyanda za juu kusini amesema kazi ambayo imefanywa na serikali kupitia Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyama Pori Tanzania (TAWA) ni kuhifadhi, kulinda na kusimamia Bonde la akiba la Kilombero ili kuhakikisha mtiririko wa yanayokwenda katika bwawa hilo unalindwa.
Aidha, amesema, hadi sasa wameweza kudhibiti shughuli za kijamii hususan ufugaji na kilimo zinazofanyika katika eneo la hifadhi nje na ndani kufikia asilimia 88 hii ni kutokana na Serikali kuongeza Askari, boti Pamoja na magari.
Naye Kaimu Kamishna Msaidizi Ulinzi wa Wanyama pori Alfonce Ambroce amesema katika pori hilo la Kilombero ulinzi umeongezeka na wananchi wameshaanza kuondoka kwa hiari eneo hilo la hifadhi baada ya kupata uelewa wa kutosha kuhusu faida ya pori hilo.
Pia ametoa wito kwa wanchi ambao bado hawajaanza kuchukua maamuzi ya kuondoka katika eneo la hifadhi waanze mara moja kwa sababu Serikali imedhamiria kuhakikisha kwamba eneo la hifadhi la Pori la akiba Kilombero linatuzwa.
MWISHO.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro
Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO
Simu: +2550232934305
Simu: +255766828252
Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz
Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.