Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima amekubaliana na uwekezaji wa DP WORLD unaotarajiwa kufanywa katika bandari ya Dar es Salaam kwani amesema utaongeza uchumi wa Taifa na maslahi mapana hapa nchini.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Malima akielezea fursa zilizopo ndani ya Mkoa wa Morogoro wakati wa mahojiano na Wasafi Media.
Mhe. Malima ameyasema hayo Julai 10 mwaka huu wakati wa mahojiano na Wasafi katika kipindi chake Cha Habari za Asubuhi (Good mornging) ikiwa ni muendelezo wa programu yao ya WEKEZA NA TANZANIA YA SAMIA yaliyofanyika Ofisini kwake.
Mkuu huyo wa Mkoa amesema kuwa kimsingi bandari ndio kitovu cha uchumi kwa kuwa fursa nyingi za kiuchumi zinapatikana hapo, hivyo anawashangaa watu wanaobeza makubaliano yaliyofanyanwa na serikali juu ya uendeshaji wa bandari hiyo.
Hapa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Malima akiwa na mwandishi wa Wasafi Media Bw. Maulid Kitenge wakati wa mahojiano.
"...na lazima uelewe bandari ni kitovu cha uchumi wa Tanzania, inapofanya kazi vizuri mambo mengi yanafunguka...unapozungumzia DP WORLD ni oparetors ambao wako duniani kote sasa kama una issue na mkataba zungumzia mkataba sio uwezo wa DP WORLD..." amesema Mhe. Adam Malima.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Malima (katikati) akiwa na waandishi wa habari kutoka kushoto ni Bw. Gerard Hando, Zembwela, kulia Bw. Charles William, pamoja na Bi. Salma Dacotha.
Aidha, amesema suala hilo la bandari halihitaji mambo ya siasa kwa kuwa Mkoa wa Morogoro ni miongoni mwa wanufaika wa bandari hiyo, hivyo amewataka wanasiasa kutoa maoni ya kuboresha mkataba kwa manufaa ya watanzania.
Katika hatua nyingine, Mkuu huyo amesema Mkoa wa Moroogoro ni Mkoa wa kimkakati kutokana na uwepo wa mambo mbalimbali muhim hapa nchini kama vile uzalishaji wa chakula, nishati na upatikanaji wa maji.
Katika suala viwanda, Mhe. Adam Malima amesema Mkoa umeweka mikakati ya kutangaza fursa za uwekezaji wa viwanda kwa kuwa malighafi za viwanda hivyo zipo za kutosha ndani ya Mkoa huo. Sambamba na hayo amepongeza juhudi zinazofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuweka mazingira mazuri ya biashara na kuwavutia wawekezaji.
Pia, Mkuu huyo wa Mkoa amewakaribisha wawekezaji, kuja kuwekeza Morogoro katika sekta ya madini kutokana na uwepo wa madini mbalimbali yenye thamani yakiwemo madini ya vito, dhahabu na grafaiti.
MWISHO.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro
Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO
Simu: +2550232934305
Simu: +255766828252
Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz
Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.