Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutenga fedha zaidi ya shilingi bilioni 10 kwa ajili ya kuwezesha ujenzi wa shule za miradi ya BOOST.
Mhe. Malima ametoa Shukrani hizo leo Disemba 30, 2023 wakati wa kikao kazi cha Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais -TAMISEMI Mhe. Mohamed Omary Mchengerwa na Wahe. Wakuu wa Mikoa wote Tanzania Bara kilichofanyika kupitia Video Conference.
Kikao hicho kililenga kutoa taarifa ikiwa ni Pamoja na namna Wahe. Wakuu wa Mikoa hao walivyojipanga katika kuwapokea wanafunzi watakaoanza masomo ya darasa la kwanza na watakaoanza Kidato cha kwanza hapo Januari, 2024.
Mhe. Malima Pamoja na Kumshukuru Rais kwa fedha nyingi zilizopokelewa Mkoani humo na kuelekezwa katika Sekta ya Elimu bado amempongeza kwa dhati kwa kutoa zaidi ya shilingi Bilioni 10 kwa ajili ya ujenzi wa shule za Boost ambapo hadi sasa amesema kuna shule 17 za Mradi wa Boost zenye jumla ya madarasa 196 na kila Halmashauri ndani ya Mkoa huo imenufaika na mradi huo.
“…..Namshukuru sana Rais pamoja na Serikali yake kwa sababu miradi hii imejielekeza kwenye kukamilisha na kupunguza uhaba wa madarasa…” amesema Mhe. Adam Malima.
Akitoa taarifa ya wanafunzi watakaoanza kidato cha kwanza, Mkuu huyo wa Mkoa amesema waliofanya mtihani ni wananfunzi 71,922 na waliofaulu ni wanafunzi 56,604 sawa na asilimia 78.70 na akamhakikishia Waziri wa TAMISEMI kuwa wanafunzi wote 56,604 atahakikisha wanakwenda kuanza masomo yao ya kidato cha kwanza tena kwa wakati.
akibainisha zaidi, Mkuu wa Mkoa amesema jumla ya wanafunzi hao 56,604 waliofaulu Kwenda sekondari, wanafunzi 51 watakwenda shule za vipaji maalum, wanafunzi 62 watakwenda shule ya mafuzo ya mali, na wanafunzi 83 watakwenda shule za Bweni. Sambamba na hizo, wanafunzi 403, watakwenda shule teule, wanafuzi 98 watakwenda shule za mahitaji maalumu na wanafuzi 55907 watakwenda shule za kutwa.
Akithibitisha taarifa yake kwa Waziri, Mhe. Adam Malima amesema Mkoa huo umejipanga kukamilisha shule mpya za sekondari 9, zenye vyumba vya madarasa 101 na pia unakamilisha madarasa 38 ya mradi wa SEQUIP yenye jumla ya shilingi bilioni 17.2 kwa miradi mbalimbali ya SEQUIP.
Mhe. Adam Malima amesema, Mkoa unaendelea kujielekeza kwenye kuongeza ufaulu wa wanafunzi ili kuboresha zaidi asilimia ya ufaulu kutoka asilimia 78.70% ya mwaka huu na kupanda zaidi.
MWISHO.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro
Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO
Simu: +2550232934305
Simu: +255766828252
Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz
Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.