Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Martine Shigela amemshukuru Mhe. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuweza kuwaondolea wananchi wa Mkoa huo kero ya upatikanaji wa maji safi na salama kwa kipindi hiki kifupi Cha Uongozi wake.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Martine Shigela akitoa salam za pongezi kwa Mhe. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Kongamanp la wadau wa Elimu wa Mkoa huo Julai 2 Mwaka huu katika ukumbi wa Chuo Kikuu cha Kiislam cha Morogoro (MUM) Mkoani humo.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro Bi. Mariam Mtunguja akimkaribisha Mkuu wa Mkoa huo ili azungumze na wadau wa elimu katika Kongamano hilo.
Martine Shigela amesema hayo Julai 2 mwaka huu katika kongamano la wadau wa elimu la kufanya tathmini ya sekta ya Elimu na kumpongeza Mhe. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lililofanyika katika ukumbi wa Chuo cha Kiislam cha Morogoro.
Mhe. Palamagamba Kabudi Mbunge wa Jimbo la Kilosa akizungumza wakati wa kutoa pongezi hizo.
Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Albart Msando akiteta jambo na Mwenyekiti wa Chama Tawala Mkoa wa Morogoro Ndg. Doroth Mwamsiku wakati wa Kongamano hilo.
Mkuu huyo wa Mkoa amebainisha kuwa kipindi cha mwaka mmoja wa uongozi wa Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan ni cha mafanikio makubwa kwenye Sekta mbalimbali hapa nchini hasa katika Sekta ya maji ambapo zaidi ya shilingi 8bil. zimetumika kwa mwaka wa fedha wa 2021/2022 katika ujenzi miradi ya kimkakati inayolenga kuwaondolea kero hiyo wananchi wa Mkoa wa Morogoro.
Katibu Tawala Msaidizi upande wa Elimu wa Mkoa huo Bi. Germana Mung'aho akisoma taarifa ya uwepo wa wanafunzi wa shule za Msingi na Sekondari Mkoani Morogoro.
Zawadi zilizoandaliwa kwa ajili ya Halmashauri, Shule na Wanafunzi waliofanya vizuri kitaaluma Mkoani Morogoro.
Aidha, ameongeza kuwa Miradi ya maji inayotarajiwa kujengwa katika miji 28 nchini kote, Mkoa wa Morogoro ni mnufaika wa mradi mmojawapo utakaotekelezwa Katika Mji Mdogo wa Ifakara ambapo ukamilikaji wake utachangia kwa kiasi kikubwa kukomesha kabisa kero ya Maji kwa wakazi wa maeneo hayo.
“Kwa mwaka wa fedha ulioisha ni zaidi 8Bil. zimetumika katika kutekeleza miradi mbalimbali ya maji Mkoa mzima kama sehemu ya kusogeza huduma kwa wananchi” amesema Shigela.
“Na zaidi ya Tsh. 50Bil. zimetengwa kuanza kujenga mradi mkubwa wa maji katika Hamashauri ya Mji mdogo wa Ifakara ambapo ni moja ya miradi inaotarajiwa kutekelezwa katika Miji 28 nchi nzima” ameongeza Shigela.
Katika hatua nyingine Martine Shigela ameweka wazi kuwa kwa upande wa elimu bila malipo Mkoa wa Morogoro kwa kipindi cha mwaka mmoja umepokea zaidi ya 14Bil. kuweza kugharamia elimu bila malipo kwa Shule za Msingi na Sekondari.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Martine Shigela akipokea zawadi ya usimamizi bora na kama mdau mkubwa wa elimu kutoka kwa Katibu Tawala wa Mkoa huo Bi. Mariamu Mtunguja pamoja na Katibu Tawala Msaidizi upande wa Elimu Mkoa wa Morogoro Bi. Germana Mun'gaho.
Naye Mwenyekiti wa Chama Tawala CCM Mkoa wa Morogoro Ndg. Doroth Mwamsiku amesema Chama hicho Mkoani humo kinafurahishwa na mwenendo wa utendaji wa walimu katika kuendelea kuwapatia maarifa watoto wa Kitanzania ili kujenga taifa lililobora na lenye utashi.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Morogoro Ndg. Doroth Mwamsiku akiwasilisha salam za chama wakati wa Kongamano la wadau wa elimu la Kumpongeza Mhe. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Nao wadau wa kada hiyo akiwemo Mwalimu Mipiana Donard Kilasile ambaye ni Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Lukwiva ametoa wito kwa walimu na watendaji wengine kusimamia na kufuatilia vema ufundishaji wa watoto ili kuweza kufikia malengo ya kuinua Mkoa huo kielimu.
Mwalimu Mipiana Donard Kilasile ambaye ni Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Lukwiva akizungumza mara baada ya Kongamano la wadau hao.
Baadhi ya wadau wa elimu Mkoani Morogoro wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Mkoa huo akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Martine Shigela.
MWISHO.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro
Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO
Simu: +2550232934305
Simu: +255766828252
Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz
Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.