Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Martine Shigela amepongeza ushirikiano uliopo baina ya uongozi wa Kata ya Bwakila Chini, Vijiji vya Mbwade na Duthumi, wazazi na walimu wa Shule za msingi Bonye na Duthumi kwa kupunguza changamoto ya wanafunzi kukaa chini kwa kutengeneza madawati, meza na viti.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Martine Shigela akizungumza na wananchi wa Kata ya Bwakila chini Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro wakati wa ziara yake iliyofanyika Juni 24 mwaka huu'.
Martine Shigela ametoa pongezi hizo Juni 24 mwaka huu wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua miradi ya maendeleo pamoja na kutatua kero za wananchi katika Kata ya Bwakila Chini. Ikiwa ni muendelezo wa ziara yake katika Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro.
Mkuu wa Mkoa Martine Shigela akikata utepe kuashiria kuzindua madawati 400 yaliyotengenezwa kwa ushikiriano wa wanavijiji viwili vya Mbwade na Duthumi kwa gharama ya Tsh. 9.5mil.
Martine Shigela amesisitiza kuwa mambo yanayohusu maendeleo yanaanza na wananchi wenyewe, hivyo amewapongeza wananchi wa Kata ya Bwakila Chini kwa kuweza kutengeneza madawati 400, meza 12 na viti 12 vya walimu kwa gharama ya shilingi 9.5 Mil. Kwa njia ya Michango yao wenyewe na kuokoa zaidi ya shilingi 28mil ambazo zingegharimiwa na Serikali.
“Kwa hiyo mlilolifanya ni jambo kubwa, ni jambo la heshima na jambo la kimaendeleo ambalo kiongozi yoyote ukimleta hapa atafarijika kwa hili, wanabwakila mmefanya jambo kubwa la kimaendeleo hongereni” amesema Shigela.
Katika hatua nyingine Mkuu huyo wa Mkoa amepiga marufuku na kutoa onyo kali kwa baadhi ya walimu wanaowatumikisha wanafunzi ili kuwafanyia biashara ama kuwauumia kukima katika mashamba yao wakati Serikali inayumia fedha nyingi kuwasomesha bila malipo kwa lengo la kutaka wanafunzi wasome kwa utulivu.
Mkuu a Wilaya ya Morogoro Albart Msando akimkaribisha Mkuu wa Mkoa wa Morogoro kuzungumza na wananchi wa Kata ya Bwakila chini Juni 24 mwaka huu.
Kwa upande wake diwani wa Kata hiyo Bw. Amiri Mihungo amemuhakikishia Mkuu wa Mkoa kuwa zoezi la utengenezaji wa madawati ni endelevu kwani wameanza na Vijiji viwili vya Mbwade na Duthumi lakini ni matarajio yao kufikia Vijiji vyote vinne vya Kata hiyo ili kuweza kupunguza au kuondoa kabisa changamoto za wanafunzi kukaa chini.
Akisoma taarifa ya utekelezaji wa mradi huo Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Bonye Bw. Gift Sadrudin Meghji amesema utekelezaji wa mradi huo ni sehemu ya kuunga mkono azma ya Serikali ya awamu ya sita ya kuhakikisha wanafunzi wanapata elimu iliyo bora kwa kuwaboreshea mazingira ya kusomea na kufundishia.
Nao wananchi wa Kata hiyo wakieleza changamoto zinazowakabili akiwemo Bi. Maria Kaweche ambaye ni mkazi wa Kijiji cha Duthumi ameeleza changamoto ya baadhi ya walimu kuwayumikisha wanafunzi kwa kuwafanyia biashara zao na kilimo Katika mashamba yao wakati wanatakiwa kuwa darasani, kero ambayo Mkuu wa Mkoa tayari alishaitolea maelekezo ya kupiga marufuku.
Baadhi ya wananchi wa Kata ya Bwakila chini waliohudhuria katika mkutano wakati wa ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Martine Shigela katika Kata hiyo Juni 24 mwaka huu.
MWISHO.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro
Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO
Simu: +2550232934305
Simu: +255766828252
Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz
Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.