• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
Mkoa wa Morogoro
Mkoa wa Morogoro

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Morogoro

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Maelezo ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Sehemu na Vitengo
      • Utawala na Rasilimali
      • Serikali za Mitaa
      • Uhasibu na Fedha
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Sheria
      • TEHAMA
      • Afya
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Kitengo cha Habari na Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Morogoro
    • Mvomero
    • Gairo
    • Kilosa
    • Kilombero
    • Ulanga
    • Malinyi
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Morogoro
    • Morogoro DC
    • Mvomero
    • Gairo
    • Ulanga
    • Malinyi
    • Mlimba
    • Ifakara Mji
    • Kilosa
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uchimbaji wa Madini
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
    • Huduma za Ugavi
  • Machapisho
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
    • Fomu Mbalimbali
    • Ripoti mbalimbali
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Videos
    • Hotuba
    • Picha

RC MOROGORO ATANGAZA VITA KWA WAKANDARASI 'VISHOKA'.

Posted on: October 23rd, 2022

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Fatma Abubakar Mwassa ametangaza vita dhidi ya wakandarasi wanaofanya kazi Mkoani humo wasiotekeleza kazi zao kwa ubora unaotakiwa ambao amewaita ‘vishoka’ huku akiwataka mara watakaposikia taarifa hizi waanze kufunga virago au kubadili utendaji wao wa kazi.

Wabunge wa Mkoa wa Morogoro nao walihudhuria kikao hicho cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa (RCC).

Fatma Mwassa ametoa agizo hilo kwa wakandarasi wa aina hiyo Oktoba 23 mwaka huu wakati akifungua kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa (RCC) kilichofanyika Hoteli ya Morena katika Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro.

Amesema, ujenzi wa barabara nyingi ndani ya Mkoa huo zimejengwa chini ya kiwango na tatizo kubwa likiwa ni uwepo wa wakandarasi wengi wasiotekeleza kazi zao kwa ubora unaohitajika kwa mujibu wa mikataba wanayoisaini na kuagiza wakandarasi hao kutolipwa fedha wasipofanya kazi hizo kwa tija.

Mkuu wa Wilaya ya Kilombero Hanji Godigodi akitoa maoni yake wakati wa majadiliano kwenye kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa (RCC), kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Ulanga Ngollo Malenya akiwa pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Mvomero Halima Okash.

“sasa mimi nitangaze tu, nimetangaza vita na Wakandarasi vishoka, huko waliko taarifa hizi zikiwafikia waanze kufunga virago waondoke Morogoro, sababu hakuna Mkandarasi atakayelipwa bila kufanya kazi yenye tija”. amesema Fatma Mwassa.

Katika hatua nyingine, Mkuu huyo wa Mkoa amesikitishwa na ujenzi wa daraja lililojengwa Wilayani Kilombero likiwa chini ya kiwango na kuagiza daraja hilo kubomolewa haraka na kujengwa upya kabla yeye hajafika kulikagua vinginevyo mkandarasi anayehusika na ujenzi huo atachukuliwa hatua Kali za kisheria.

Wajumbe wa Kikao hicho wakiwa katika mjadara wa upatikanaji wa Maji hususan katika Manispaa ya Morogoro Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira (MORUWASA) Mkoa wa Morogoro Mhandisi Tamimu Katakweba amesema hali ya upatikanaji wa maji katika Manispaa hiyo umefikia asilimia 48 chini ya lengo la Serikali la kufikisha upatikanaji wa Maji kwa asilimia 95 Mijini huku akitaja mikakati ya kufikia kuhakikisha asilimia 95 ifikapo mwaka 2025.

Aidha, ameongeza kuwa kwa sasa Manispaa hiyo inategemea maji kutokanBwawa la Mindu kama chanzo kikuu cha maji ambapo kwa Sasa uzalishaji wake ni lita milioni 35 hadi 37 kwa siku huku mahitaji yakiwa lita milioni 73.

Wakijadili suala la utunzaji mazingira na vyanzo vya maji, Wajumbe wa kikao hicho akiwemo Mbunge wa Jimbo la Kilosa Prof. Paramagamba Kabudi ameshauri Mkoa kuwa na Mkakati wa kuhifadhi mazingira kwa kuwa ni Mkoa pekee wenye vyanzo vingi vya Umeme unaotokana na Maji kwa asilimia zaidi ya tisini.

Mkuu wa Mkoa Fatma Mwassa akishuhudia utiaji wa saini mkataba wa lishe bora iliyoboreshwa, saini hiyo imewekwa na Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Albert Msando.

Amesema, Mkoa wa Morogoro unapitiwa na mito inayopeleka maji Bwawa la Mwalimu J. K. Nyerere na kuna vyanzo vya maji yanayokwenda Mikoa ya Pwani na Dar es Salaam hivyo Mkoa unatakiwa kuwa na Mkakati maalum kwa ajili ya kulinda mazingira hususan kwenye vyanzo vya Maji ili bwawa la Mwalimu Nyerere liwe endelevu na Mikoa inayotegemea maji ambayo vyanzo vyake ni kutoka Morogoro iweze kupata maji yenye uhakika.

Aidha, wajumbe wa kikao hicho wameshauri zao la Mkonge kuongezwa na kuwa zao la Kimkoa baada ya mazao mawili ya Mpunga na Miwa kwa maana ya uzalishaji wa Sukari kwa kuwa hali ya hewa ya Mkoa huo na Ardhi vinaruhusu zao hilo kustawi.

Makatibu Tawala wa Wilaya walikuwa ni miongoni mwa wajumbe waliohudhuria kikao hicho.

MWISHO.

Matangazo

  • MATOKEO YA DARASA LA SABA 2024 October 30, 2024
  • TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI. May 13, 2025
  • View All

Habari Mpya

  • MAFUNZO YA AMIS NA TAUSI YATOLEWA MKOANI MOROGORO.

    May 21, 2025
  • MAFUNZO YA AMIS NA TAUSI YATOLEWA MKOANI MOROGORO.

    May 21, 2025
  • Zaidi ya Mil. 125 zachangwa kupitia chakula cha hisani kukarabati Hospitali ya Rufaa Morogoro.

    May 18, 2025
  • RC MALIMA ASHIRIKI MATEMBEZI YA HISANI, ASEMA HOSPITALI YA RUFAA INAHIMILI WAGONJWA.

    May 17, 2025
  • View All

Video

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima akikagua ujenzi wa jengo la ofisi mpya ya Mkuu wa Mkoa.
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Maelezo ya Mkoa
  • Tangazo la Zabuni
  • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
  • Hotuba
  • Taarifa kwa Umma

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Tanzania
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • TAMISEMI
  • Ikulu
  • Katibu Mkuu Kiongozi
  • Tovuti ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro

    Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO

    Simu: +2550232934305

    Simu: +255766828252

    Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.