Mhe. Adam malima akitoa pole kwa viongozi wa shule yasekondari Compassion mara baada ya kutembelea shuleni hapo kujionea athari zilizosababishwa na moto. kulia kwake Mkuu wa Wilaya ya Kilombero Mhe. Danstani Kyobya, na kushoto kwake ni Katibu Tawala Mkoa wa Morogoro Dkt. Mussa Ali Mussa.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima ametembelea shule ya Sekondari ya Compassion iliyopo Kata ya Sanje Wilayani Kilombero Mkoani humo na kutoa pole kwa wamiliki wa shule hiyo huku akiagiza mabweni matatu yaliyoteketea kwa moto kubomolewa mara moja na kujengwa upya kwa kuzingatia ushauri wa jeshi la zima moto na uokoaji.
Hapa Mhe. Adama Malima anakagua baadhi ya majengo yaliyopo shuleni hapo.
Mhe. Adam Malima ametoa agizo hilo Juni 4 mwaka huu alipofika eneo la tukio ili kuona athari ya moto ulivyoteketeza mabweni hayo na mali mbalimbali za shule hiyo inayomilikiwa na mapadre Wamissionari wa Huruma (Missionaries of Commpassion) na kutoa pole.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Malima aakizungumza na viongozi wa shule pamoja na baadhi ya wajumbe wa Menejimenti ya Mkoa walioambatana nae.
Baada ya kutembelea mabweni na majengo mengine yaliyoteketea na kujionea hali halisi Mhe. Adam Malima akatoa maagizo kwa watendaji wake kubomoa majengo hayo na kuanza kuyajenga upya kwa kufuata kanuni lengo ni kuwalinda wanaoishi humo endapo tukio kama hilo litatokea kwa kuweka milango mingi na kutounganisha majengo mengi ili kulinda majengo mengine yasiungue endepo jengo moja litashika moto.
"sasa hivi ni kwamba mtakapokuwa mnajenga ni lazima mpate Consultation kutoka kwa watu wa Fire Depatment ili wakwambieni zile exit strategies na hiyo michoro yenu ni lazima iwe na milango, huwezi kuwa na mlango mmoja kama hivi, ni lazima kuwa na milango mingi" amesema Mhe Adam Malima.
Aidha, amewaagiza jeshi la zimamoto na Uokoaji kupita mabweni mengine kuyakagua na kuyaboresha endapo kuna uhitaji huo na kuweka vizimia moto (Fire existinguisher) lengo ni kuokoa uhai wa watu endapo matukio hayo yatatokea.
Baadhi ya majengo yaliyoteketea kwa moto.
Katika hatua nyingine Mkuu wa Mkoa amemuagiza Mhandisi wa Mkoa wa Morogoro Eng.ezron Kilamhama kusimamia majengo hayo watakapokuwa wanajenga ili michoro hiyo ifanane na michoro ya mabweni ya Wizara ya Elimu ambayo yana milango ya kutosha ya kutokea wanafunzi endapo kuna matukio kama hayo.
kwa upande wake Kamanda wa jeshi la zimamoto Wilaya ya Kilombero Ispekta Haji Mohamed Madulika amesema katika tukio hilo hakuna madhara ya kibinadamu yaliyotokea huku akibainisha kuwa moto huo ulidhibitiwa na jeshi hilo majira ya saa 11:00Pamoja na kuwa chanzo cha moto huo hadi sasa bado hakijajulikana ametoa wito kwa wananchi kuitumia namba ya dharura ya kupiga bure wakati wanapopatwa na majanga ili waweze kupata usaidizi wa haraka kutoka kwa jeshi hilo ambayo ni 114.
Nae msimsmizi wa shule hiyo Paroko wa Parokia ya Bikira Maria Mpalizwa Mbinguni ya Msolwa Ujamaa, Padre George Alexis amemshukuru Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Malima kwa kuacha shughuli zake nyingi na kuamua kwenda kuwapa pole, hivyo amemshukuru pia Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuwapa watendaji wanaojali wananchi wao na kuahidi kuendelea kufanya kazi pamoja.
Padre George Alexis (kushoto) Msimamizi wa shule ya Compassion akitoa neno la shukrani kwa Mkuu wa Mkoa Mhe. Adama Malima.
Mwenyekiti wa wa Bodi ya shule hiyo Bw. Joseph Peter Liganzio amesema hadi sasa bado hawajapata gharama halisi ya hasara iliyopatikana kufuatia ajali hiyo ya moto, hata hivyo anawashukuru wananchi na viongozi wote waliowakimbilia katika tukilo hilo kubwa.
kwa mujibu wa Mkuu wa Shule ya Compassion Sekondari, sister Bindu Michael Palapparambil amebainisha makadirio ya athari za ajali hiyo ya Moto iliyotokea Juni 2 mwaka huu majira ya saa 6:40 Mchana kuwa ni pamoja na uharibifu wa Jengo lenye mabweni matatu, uharibifu wa chumba cha Mkuu wa shule kikiwa na fedha taslimu na nyaraka muhim, uharibifu wa chumba na Ofisi ya mwalimu.
Baadhi ya mali za wanafunzi zilizoteketea kwa moto.
Vingine ni uharibifu wa chumba cha Msimamizi, uharibifu wa chumba cha kushonea na vifaa vyake, uharibifu wa chumba cha wageni, uharibifu wa store ya chakula na vyakula, uharibifu wa Tenki la maji pamoja na uharibifu wa hati za kusafiria na nyaraka nyingine muhimu.
Shule ya sekondari ya Compassion inayomilikiwa na mapadre Wamissionari wa Huruma kwa kushirikiana na masista wa Roho Mtakatifu ilianzishwa mwaka 2009 ina jumla ya wanafunzi 311 wasichana 149, wavulana 162 na hakuna mwananfunzi aliyejeruhiwa.
Mhe. Adam Kighoma Malima ametoa mchango wa shilingi 1,000,000.00 kwa ajiri ya ujenzi wa mabweni yaliyoteketea kwa moto ili ifikapo Julai mwaka huu wanafunzi wanaporejea shuleni hapo waweze kuendelea na masomo yao kwa utiulivu.
MWISHO.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro
Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO
Simu: +2550232934305
Simu: +255766828252
Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz
Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.