Mhe. Fatma Mwassa Akifungua kikao cha Bodi ya Barabara leo tarehe 6 Mwezi wa Tatu Ukumbi wa Hoteli ya Morena
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Fatma Mwassa amewaagiza Meneja wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) na Wakala wa Barabara Vijini na Mijini (TARURA) Mkoa wa Morogoro kuwachukulia hatua za mapema wale wote wanaojenga au kufanya shughuli zao kwenye hifadhi za barabara ili kuepuka usumbufu wa kubomolewa wakati nyumba au majengo yao yakiwa yamekamilika.
Meneja wa Bodi ya Barabara (Eng Alinanuswe Kyamba) Akitoa Tarifa ya utekelezaji wa Miundombinu ya Barabara Mkoani Morogoro
Mhe. Fatma Mwassa ametoa agizo hilo Machi 6 mwaka huu wakati akifungua kikao cha Bodi ya barabara cha Mkoa kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa hoteli ya Morena iliyopo katika Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro.
Mhe. Fatma Mwassa amewaagiza Meneja wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) na Wakala wa Barabara Vijini na Mijini (TARURA) Mkoa wa Morogoro leo.
Amesema, hakuna mantiki kuwaacha wananchi wakiendelea na ujenzi kwenye hifadhi za barabara hadi wanakamilisha ujenzi na kisha kuja kuwabomolea wakiwa wamekamilisha, ni vema kuwachukulia hatua mapema kwa kusitisha ujenzi wakiwa katika hatua za msingi na kisha kutoa Elimu ya kutojenga maeneo hayo ili kuepuka usumbufu wa kubomolewa majengo yao.
“...kwenye hili niwaombe sana TARURA na TANROADS mtu anapoanza tu kujenga anatakiwa kubomolewe pale pale ...ananza tu kuchimba msingi mnabomoa na kumuelimishwa kwamba hapa hapaswi kujenga...” amesema Mhe. Fatma Mwassa.
Aidha, Mkuu huyo wa Mkoa ameagiza kuchukuliwa hatua za kisheria wale wote wanaohujumu miundombinu ya barabara zikiwemo alama za barabarani, vivuko, na kingo za madaraja ya chuma ambapo hadi sasa takribani alama 19 zimeibiwa kwenye barabara mpya ya Ludewa – Kilosa Wilayani.
Waheshimiwa Wakuu wa Wilaya kwenye kikao cha Bodi ya Barabara Leo ukumbi wa Morena
Mkuu huyo wa Mkoa amesema niwajibu wa kila mwananchi kulinda, kutunza miundo mbinu ya barabara, vivuko na alama za barabarani zinazowekwa ili alama hizo ziweze kudumu kwa muda mrefu.
“...naagiza hatua kali za kisheria zichukuliwe kwa yeyote atakaebainika kuhujumu miundombinu ya barabara zetu au kwa uharibifu wa aina yoyote ile...” amesema Mhe. Fatma Mwassa.
Katika hatua nyingine Mkuu huyo wa Mkoa amewaagiza Meneja wa TANROADS na TARURA kuwatumia wakandarasi wa ndani ya MKoa (wazawa) wenye sifa za kutengeneza barabara ili kukuza uchumi wa Mkoa huo.
Hata hivyo ametoa rai kwa Wakandarasi wote wanaopewa kazi za ujenzi wa miundombinu katika Mkoa huo kuhakikisha wanafanya kazi kwa weredi na kukamilisha kazi zao kwa mujibu wa mikataba waliyosaini.
Katibu Tawala Mkoa wa Morogoro Mussa Ali Mussa
MWISHO
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro
Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO
Simu: +2550232934305
Simu: +255766828252
Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz
Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.