Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Loata Ole Sanare amemuagiza Kamanda wa Jeshi la Polisi Wilaya Kilombero kuwatia mbaloni wafanyabiashara watatu kwa tuhuma za kuhujumi uchumi wa nchi.
Loata ametoa agizo hilo Januari 7 mwaka huu ikiwa ni siku ya pili ya ziara yake ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa Shule za Sekondari kwa ajili ya wanafunzi wa kidato cha kwanza wanaotarajiwa kuanza masomo januari hapo 11, 2021.
Aidha, Kukamatwa kwa wafanyabiashara hao kumetokana na madai ya kuuza bidhaa mbali mbali bila kuwa na leseni kutoka kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) hivyo kuhujumu uchumi wa nchi licha ya Serikali inayoongozwa na Dkt. John Pombe Magufuli Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutilia Mkazo katika suala nzima la ulipaji kodi.
Mkuu huyo wa Mkoa amebinisha baadhi ya bidhaa ambazo wafanyabiashara hao wamekuwa wakiuza bila kulipa kodi kwa Mamlaka husika, kuwa ni pamoja na Saruji katika maduka ya kuuza vifaa vya ujenzi ambapo wamekuwa wakiuza bidhaa hiyo bila kutoa risiti kwa wanunuzi.
Sambamba na hayo, Loata ametoa agizo kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania - TRA kufanya utafiti juu ya mfanyabiashara Didas Kessy Paul juu ya mifuko ya saruji inayoingia na kutoka, kutokana na kuchanganya mifuko isiyo na vigezo katika sehemu moja huku ikisemekana kuuzwa kwa wananchi.
‘’TRA Naenda vijijini nikirudi hapa nipate proper record ya huyu mfanyabiashara anaingiza mifuko mingapi na anatoaje’’ amesema Sanare
Mkuu wa Wilaya ya Kilombero Ismail Mlawa, amekiri kuwepo kwa wafanyabiashara ambao hawalipi kodi kwa muda mrefu huku akimtaja mmoja wa wafanyabiashara hao Ndg Robert Mbilinyi amekuwa mmoja wa wafanyabiashara wasumbufu katika ulipaji kodi ndani ya Wilaya hiyo hali iliyopelekea kutozwa faini ya zaidi Mil.10 miezi miwili iliyopita.
Naye, Afisa Mapato Wilaya ya Kilombero Amani Timotheo ametaja majina ya wafanyabiashara ambao wamekuwa wakifanya biashara bila kulipa kodi kuwa ni James Mwaisungu ambaye anajihusisha na uuzaji wa vifaa vya pikipiki na Ndg. Robert Mbilinyi muuzaji wa saruji.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro
Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO
Simu: +2550232934305
Simu: +255766828252
Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz
Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.