Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Fatma Mwassa amewataka viongozi Mkoani humo kuunganisha na kuelekeza nguvu zao katika kulinda Mazingira katika maeneo wanamoishi. Mhe. Fatma Mwassa ametoa agizo hilo Novemba 3 mwaka huu, kwenye kikao kazi cha viongozi wa Mkoa na Wilaya kilichofanyika katika ukumbi wa Magadu Katika Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro.
Mkuu wa MKoa wa Morogoro Mhe. Fatma Mwassa (katikati) akiongoza Kikao Kazi cha viongozi wa ngazi ya juu kabisa ndani ya Mkoa huo wakiwemo viongozi wa Kamati za Ulinzi na Usalama ya Mkoa na Kamati za Ulinzi na Usalama za Wilaya zote za Mkoa huo. Kushoto kwake ni Katibu Tawala wa Mkoa huo Dkt. Mussa Ali Mussa.
Mkuu wa Mkoa amesema Mkoa huo unashika nafasi ya nne katika uzalishaji wa chakula hapa nchini, hivyo ikiwa mazingira ya Mkoa huo yataharibiwa wakulima hawataweza kulima na kupata mazao kwa kiwango kile ambacho nchi inatalajia. “...nasema hivi, suala la mazingira ni letu sote... ‘no compromise’...” amesema Fatma Mwassa.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Fatma Mwassa (katikati waliokaa) akiwa kwenye picha ya pamona na Wakuu wa Wilaya wa Mkoa huo na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa baada ya Kikao cha Viongozi wa Mkoa na Wilaya.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Fatma Mwassa (katikati waliokaa) akiwa kwenye picha ya pamoja na Sekretarieti ya Mkoa na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa baada ya kikao cha Mkuu wa Mkoa na Viongozi wa Mkoa na Wilaya.
Aidha, Mkuu wa Mkoa ametaja athari zinazotokana na uharibifu wa mazingira zikiwemo upungufu wa maji katika mto Ruvu ambao unatokana na uharibifu mkubwa wa mazingira katika mikoa ya Pwani na Morogoro ambao unatokana na uwepo wa shughuli za kibinadam zinazoendelea katika vyanzo vya maji. Sambamba na hilo, Mhe. Fatma Mwassa amesema wafugaji wanaolisha mifugo yao kwenye mashamba ya wakulima wanatakiwa kuchukuliwa hatua kali kwa mujibu wa kisheria.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Fatma Mwassa akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi wa Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro.
Kwa upande wao wajumbe wa kikao hicho Alhaj Majid Mwanga ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Kilosa ameshauri kuwatumia Maafisa Tarafa katika ukusanyaji wa mapato, kutatua migogoro ya wafugaji na wakulima na hata kuleta mahusiano mazuri kati ya wananchi na Serikali yao kwa kuwa wao ni kiungo muhimu sana katika ustawi wa maendeleo ya Taifa letu.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Fatma Mwassa akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga.
Nae Mkuu wa Wilaya ya Gairo Mhe. Jabir Makame amesema msingi mkuu wa utekelezaji wa maazimio yote ya kikao hicho ni mahusiano mazuri na mshikamano wa viongozi wa Mkoa, Wilaya, Halmashauri na wananchi kwa ujumla, hivyo changamoto zote zinazowakabili wananchi zitatatuliwa kwa wakati.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Fatma Mwassa akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Fatma Mwassa akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Fatma Mwassa akiwa kwenye picha ya pamoja na Viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Gairo.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Fatma Mwassa akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero.
Wakurugenzi watendaji wa Halmashauri wakiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Mkoa huo Mhe. Fatma Mwassa.
MWISHO.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro
Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO
Simu: +2550232934305
Simu: +255766828252
Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz
Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.