• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
Mkoa wa Morogoro
Mkoa wa Morogoro

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Morogoro

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Maelezo ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Sehemu na Vitengo
      • Utawala na Rasilimali
      • Serikali za Mitaa
      • Uhasibu na Fedha
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Sheria
      • TEHAMA
      • Afya
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Kitengo cha Habari na Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Morogoro
    • Mvomero
    • Gairo
    • Kilosa
    • Kilombero
    • Ulanga
    • Malinyi
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Morogoro
    • Morogoro DC
    • Mvomero
    • Gairo
    • Ulanga
    • Malinyi
    • Mlimba
    • Ifakara Mji
    • Kilosa
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uchimbaji wa Madini
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
    • Huduma za Ugavi
  • Machapisho
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
    • Fomu Mbalimbali
    • Ripoti mbalimbali
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Videos
    • Hotuba
    • Picha

RC SANARE AAGIZA KUSIMAMISHWA KAZI MTENDAJI WA KIJIJI.

Posted on: March 12th, 2021

Mkuu wa Mkoa  wa Morogoro Loata Ole Sanare amemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro Bi. Rehema Bwasi kupitia Afisa Utumishi wa Halmashauri hiyo Ndg. Kelvin Luvinga kumsimamisha kazi mara moja Mtendaji wa kijiji cha Matuli Bw. Rashid Ponera ili kupisha uchunguzi wa ubadhilifu wa fedha za umma zaidi ya Shilingi Mil.100.

Loata Sanare ametoa agizo hilo Machi 11, mwaka huu wakati wa ziara ya kikazi katika Wilaya ya Morogoro ya kukagua miradi ya maendeleo pamoja na kusikiliza kero za wananchi ambapo alifika Shule ya Sekondari ya Matuli na kufanya mkutano wa hadhara  na wananchi wa Kijiji hicho.

Mkuu huyo wa Mkoa amebainisha kuwa Rashid Ponela anatuhumiwa kwa kosa la ubadhilifu wa fedha za mradi wa mkaa endelevu uliokuwa unasimamiwa na baadhi ya wanakikundi wa kijiji hicho.

‘’Sasa nikwambie tena, msimamishe leo, Mhe, Mwenyekiti wa chama yuko hapa yule mwenyekiti na yeye mchukulie hatua  za kichama nimeshagundua kuna kulindana kwingi hapa’’ amesema Loata Sanare.

Pamoja na kumsimamisha Mtendaji wa Kijiji hicho, Mkuu huyo wa Mkoa pia ameagiza Mwenyekiti wa Kijiji cha Matuli naye achukuliwe hatua za kichama kutokana na tuhuma za ubadhilifu wa fedha za mradi huo wa mkaa endelevu wa Kijiji.

Kwa upande wake Diwani wa kata ya Matuli ambaye pia ndiye Mwenyekiti wa baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya hiyo Mhe. Lucas Lemomo amesema suala la ubadhilifu wa fedha hizo aliuibua yeye kutokana na wananchi wa kijiji cha Matuli kushindwa kuchangia ujenzi wa Shule ya Msingi Matuli licha ya kuwa na mradi wa mkaa endelevu kijijini hapo.

Sambamba na hayo, Lemomo amebainisha kuwa mbali na zaidi ya Shilingi Mil. 100 zilizofanyiwa ubadhilifu, kuna Shilingi Mil. 23,500,000/= ambazo hazikuingizwa kwenye akauti ya kijiji na hazifahamiki zimetumika vipi na wapi kutokana na vielelezo husika kutowasilishwa kwenye Baraza la Madiwani baada ya kuvihitaji.

Akitoa ufafanuzi wa ubadhilifu wa fedha hiyo Afisa TAKUKURU Mkoa wa Morogoro  Emmanuel Komba amesema wahusika wa ubadhilifu wa fedha hizo wamechukuliwa hatua za kisheria ikiwa ni pamoja na kulipa sehemu ya fedha hizo ambapo hadi sasa zaidi ya Shilingi Mil. 2,000,000/= zipo kwenye akauti yao.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti wanakikundi wa mradi wa mkaa endelevu uliopo katika kijiji cha Matuli akiwemo Peter John, amempongeza Mkuu wa Mkoa Loata Ole Sanare kwa kumchukulia hatua Mtendaji wa kijiji hicho ili liwe funndisho kwa viongozi wengine.

‘’Binafsi niseme kwamba uamuzi alioufanya kiongozi wetu ni sahihi na naamini utakuwa fundisho kwa viongozi wengine, viongozi wengi wanashindwa kuwa waadilifu hali inayopelekea kutukwamisha kimaendeleo sisi wananchi’’ amesema John.

Mradi wa Mkaa Endelevu katika Kijiji cha Matuli  Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro ulianza mwaka 2016 na  utekelezaji wake  ukaanza rasmi mwaka 2017, mradi huo ulikuwa na lengo la kupiga hatua kimaendeleo na kufika mbele zaidi kwa kujitegemea kupitia Mradi huo.

 MWISHO

Matangazo

  • MATOKEO YA DARASA LA SABA 2024 October 30, 2024
  • View All

Habari Mpya

  • RC MALIMA AKEMEA ULANGUZI WA MAZAO.

    May 08, 2025
  • WAAJIRI MOROGORO WATAKIWA KUTATUA CHANGAMOTO ZA WAFANYA KAZI WAO.

    May 01, 2025
  • SERIKALI KUJENGA BARABARA YA LUPILO – MALINYI KWA KIWANGO CHA LAMI, Bil. 18 ZATOLEWA KUJENGA MADARAJA MAWILI.

    April 25, 2025
  • MWENGE WA UHURU 2025 WATAJA TUNU NNE ZA TAIFA.

    April 19, 2025
  • View All

Video

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima akikagua ujenzi wa jengo la ofisi mpya ya Mkuu wa Mkoa.
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Maelezo ya Mkoa
  • Tangazo la Zabuni
  • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
  • Hotuba
  • Taarifa kwa Umma

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Tanzania
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • TAMISEMI
  • Ikulu
  • Katibu Mkuu Kiongozi
  • Tovuti ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro

    Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO

    Simu: +2550232934305

    Simu: +255766828252

    Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.