RC MOROGORO APOKEA ZAWADI YA RAIS SAMIA
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Martine Shigela amepokea zawadi ya picha ya kuchorwa ya Rais Samia Suluhu Hassan kutoka kwa Msanii Mboya Hosiana kutoka Wilaya ya Gairo Mkoani humo akimtaka Kiongozi huyo afikishe picha hiyo kwa Rais.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Matrine Shigela (mwenye kaunda suti) akiwa katika picha ya pamoja na Msanii wa kuchora picha pamoja na Wakuu wa Wilaya za Mkoa huo na viongozi wengine wa Chama na Serikali. kulia ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Morogoro Doroth John
Shigela amepokea picha hiyo kutoka kwa msanii Hosiana Aprili 20 mwaka huu ikiwa ni alama ya kumuunga Mkoano Samia Suluhu Hassan Raisa Wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani kwa jitihada zake za kuitangaza Tanzania kimataifa kupitia filamu ya Royal Tour inayoonesha vivutio vya utalii nchini ambayo imezinduliwa hivi karibuni katika ukumbi wa Guggenheim Museum ulioko mjini New York nchini Marekani.
RC Shigela akipokea picha kutoka kwa Msanii wa kuchora picha Mboya Hosiana (kulia)
Pamoja na Mkuu wa Mkoa kuahidi kuifikisha zawadi hiyo kwa Rais kama alivyoombwa na msanii huyo, amepomngeza Msanii kwa kutumia kipaji chake kuonesha uzalendo kwa nchi yake na kwa kumuunga mkono Rais na kumzawadia shilingi milioni moja za kitanzania (Tsh. 1,000,000.00).
Mboya Hosiana akikabidhiwa kitita cha shilingi milioni moja kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Martine Shigela ikiwa ni pongezi za kumuunga Mkono Mhe. Samia kwa jitihada zake za kutangaza Utalii wa Tanzania
Aidha, Martine Shigela ameongelea jitihada zinazofanywa na Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan za Kutangaza vivutiao vya Tanzania kuwa kazi hiyo ni ya manufaa kwa nchi huku akibainisha kuwa tayari jitihada hizo zimekwisha anza kuzaa matunda kwa hifadhi za taifa zilizoko Mkoani humo kwa kuongeza watalii wanaotembelea hifadhi hizo na kwamba baadhi yake zimeshavuka lengo ikiwemo mbuga ya taifa ya Mikumi ambayo imevuka kwa asilimia 20.
“Na juzi nimetembelea kule wamenieleza kuwa mwaka huu peke yake baada ya Rais kufanya jitihada zile wameshavuka lengo la mwaka mzima kwa zaidi ya asilimia ishirini” amebainisha Martine Shigela.
Akiongea baada ya kukabidhi zawadi hiyo ya picha kwa Mkuu wa Mkoa na kupokea zawadi ya shilingi milioni moja, Msanii huyo amesema ameamua kumpa zawadi hiyo Rais ili kusaidia kampeni aliyoiazisha ya kutangaza vivutio vya Utalii vilivyopo hapa nchini na ambapo sasa vimeanza kujulikana Duniani kote.
Msanii wa Kuchora picha Mboya Hosiana kutoka Wilaya ya Gairo akiwa na picha aliyoichora
hii ndiyo picha ambayo imechorwa na Msanii Mboya Hosiana na kuomba imfikie Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kama zawadi yake kwake ya kumuunga mkono jitihada zake
Katika hatua nyingine Msanii huyo wa kuchora picha amemshukuru Mkuu wa Wilaya ya Gairo Jabil Omary Makame kwa msaada mkubwa alioutoa kwa kumsaidia kumfikia Mkuu wa Mkoa ambaye nae kwa dhamira yake njema kumzawadia shilingi milioni moja (Tsh. 1,000,000.00) huku akitoa wito kwa watanzania wote kumuunga Mkono Rais katika kampeni hiyo.
“ninaomba kwamba, hii picha imfikie mwenyewe mhusika Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ili aweze kutiwa moyo kwa kampeni aliyoianzisha na wote tuweze kujitahidi kumuunga Mkono tuweze kufikia mafanikio makubwa zaidi” amesema Msanii Mboya Hosiana.
Mkuu wa Wilaya ya Gairo Jabil Omary Makame (kushoto kabisa) akishuhudia tukio muhimu la Mkuu wa Mkoa kupokea zawadi ya Rais
MWISHO
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro
Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO
Simu: +2550232934305
Simu: +255766828252
Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz
Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.