RC SHIGELA ATOA POLE KWA MSIBA
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Martine Shigela leo Juni 14, 2022 ameitembelea familia ya ndugu Koni Ligugu ambaye ni Katibu mwenezi wa chama Tawala cha CCM Wilaya ya Malinyi aliyeondokewa na kaka yake Evodi Ligugu aliyefariki dunia Juni 11, mwaka huu na kuzikwa Juni 13 2022.
RC Shigela akiwafariji na kutoa neno la pole wafiwa
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Martine Shigela akiwafaraji wafiwa
Martine Shigela akiwa katika ziara yake ya siku tatu Wilayani Malinyi kwa lengo la kuona utekelezaji wa miradi ya maendeleo na kutatua kero za wananchi katika Wilaya hiyo amelazimika kukatisha ziara yake na kwenda kutoa pole na ubani kwa Koni Ligugu na familia yake kwa kuondokewa na kipenzi wao Evodi Ligugu
Mkuu wa Mkoa akimfariji mfiwa Bw. Koni Ligugu kushoto (Katibu mweneza wa CCM Malinyi)aliyefiwa na kaka yake Evodi Ligugu
Mkuu wa Wilaya ya Malinyi Mathayo Maselle (kushoto) pamoja mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya hiyo Mhe. Pius Mwelase(kulia) waliambatana na Mhe. Mkuu wa MKoa kutoa pole kwenye msiba huo. wa pili kulia ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro Fortunatus Muslim
RC Shigela(katikati) akiwa pamoja na Mwenyekiti wa chama cha CCM Wilaya ya Malinyi Mhe. Peter Mkanigalo wakimfariji Mfiwa
Aidha, Shigela ametoa pole kwa ndugu, jamaa na marafiki kwa kuondokewa na kipenzi chao Evodi huku akiwataka wawe na utulivu, subira na ustahimilivu katika kipindi hiki kigumu kwao na kwamba kilichobaki kwao ni kumwombea marehemu ili aweze kupumzika kwa Amani huko aliko.
Katibu wa CCM Wilaya ya Malinyi Abdulrahim Hamid akimkaribisha Mkuu wa Mkoa kusalimia na kuifariji familia ya Koni
Familia ya Bw. Koni wakiwa pamoja kwenye msiba
Katibu Mwenezi Koni Ligugu akitoa shukrani zake kwa Mkuu wa MKoa
Mkuu wa Mkoa Martine Shigela akionekana akitoa mkono wa pole kwa Katibu Mwenezi wa CCM Wilaya ya Malinyi Koni Ligugu aliyefiwa na kaka yake hivi karibuni
Bwani ametoa, bwana ametwaa, jina lake na Bwana lihimidiwe - AMINA
MWISHO
Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.