Serikali Mkoa Morogoro kupitia Ofisi ya Mkuu wa Mkoa huo inayoongozwa na Mhe. Adam Kighoma Malima imetoa ahadi kwa Gymkhana Klabu ya morogoro kuwa itatoa ushirikiano mkubwa katika kuandaa mashindano yajayo ya gofu ili kuweza kuvutia wageni wengi zaidi na kuongeza thamani ya mchezo huo katika Mkoa huo.
Ahadi hiyo imetolewa na Mhe. Malima Juni 14, 2024 wakati akifungua rasmi mashindano ya Alliance one Morogoro Open Golfu 2024 ambayo yanafanyika ndani ya siku tatu kuanzia Juni 14 hadi 16 mwaka huu katika viwanja ya Gymkhana vilivyopo Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro.
Mkuu huyo wa Mkoa amesema kupitia ufunguzi wa mashindano hayo yanaenda kuwa chachu ya kuwavutia wageni wengi kwa sababu ya uwepo wa mazingira mazuri ya hali ya hewa na uwanja mzuri wa kuchezea mchezo huo pia wageni hao baada ya kucheza mchezo huo wanaweza kwenda kutembelea vivutio vya utalii vikiwemo mbuga za wanyama, kuangalia maporomoko ya maji na vivutio vingine.
".... Ahadi yangu kwenu ni kwamba Ofisi ya Mkuu wa Mkoa itaenda kushirikiana na Gymkhana na wadau wote ili kufanya mashindano yajayo yawe makubwa zaidi kuliko haya...." Amesema Adam Malima.
Kwa upande wake Dickson Sika Mwenyekiti wa Morogoro Gymkhana Club amesema timu zote kutoka Tanzania na Nje ya Tanzania zimejitokeza kwa wingi katika mashindano hayo ambazo zikiwemo timu za watoto kutoka Kambi ya Jeshi Lugalo, timu ya Gymkhana Morogoro na timu kutoka TPC Moshi.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro
Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO
Simu: +2550232934305
Simu: +255766828252
Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz
Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.