SERIKALI YAAHIDI KUPELEKA MISAADA KWA WAATHIRIKA WA MAFURIKO MLIMBA MKOANI MOROGORO
Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan imeahidi kuwapelekea misaada mbalimbali ikiwemo chakula Pamoja na kutengeneza miundombinu ya Barabara waathirika wa mafuriko wa Mlimba Wilayani Kilombero Mkoani Morogoro.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Mhe. Jenista Mhagama (kushoto) akiwasili katika Kijiji cha Mlimba B
Ahadi hiyo imetolewa leo Aprili 11, 2024 na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, na Uratibu) Mhe. Jenista Mhagama alipofika katika Wilaya hiyo na kutembelea Kijiji cha Mlimba B ambacho kilikumbwa na mafuriko hayo hivi karibuni.
Waziri Mhagama akiongea na wananchi wa Mlimba B, Aprili, 11, 2024
Akiongea na wananchi wa Kijiji cha Mlimba B, Waziri Mhagama amesema Serikali itaendelea kushirikiana na wananchi hao katika kukabiliana na mafuriko yanayoendelea kutokea kufuatia mvua za El nino zinazoendelea kunyesha hapa nchini.
“Serikali itahakikisha huduma za Barabara, madaraja, Maji, Umeme, Mbegu, chakula na Afya zinapatikana mapema na kwa ufanisi” ameahidi Mhe. Mhagama.
Wananchi wa Mlimba B, Wilayani Kilombero Mkoani Morogoro
Mawaziri waliofuatana na Waziri Mhagama kwenye ziara ya kutembelea wananchi wa Mlimba B walioathiriwa na mafuriko
Mkuu wa Wilaya ya Kilombero Mhe. Dunstan Kyobya ndiye alikuwa mwenyeji wa ugeni huo ndani ya Wilaya yake
Ziara ya Waziri Jenista Mhagama ni mwendelezo wa ziara aliyoianza jana Aprili 10,2024 katika Wilaya za Kibiti na Rufiji Mkoani Pwani ikiwa na lengo la kuona athari za mafuriko yanayotokea hapa nchini na namna ya kukabiliana nayo lakini pia kufikisha Salam za Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa waathirika wa mafuriko hayo.
Mbunge wa Jimbo la Mlimba Mhe. Godwin Kunambi akiongea mara alipopewa fursa ya kuwasalimia wapiga kura wake
Katika Ziara hiyo Mhe. Jenista Mhagama aliambatana na Mawaziri wengine watatu Pamoja na Manaibu Mawaziri sita, Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Dkt. Jim Yonazi na Makatibu Wakuu wa Wizara tajwa Pamoja na Manaibu Makatibu Wakuu.
MWISHO
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro
Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO
Simu: +2550232934305
Simu: +255766828252
Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz
Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.