• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
Mkoa wa Morogoro
Mkoa wa Morogoro

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Morogoro

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Maelezo ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Sehemu na Vitengo
      • Utawala na Rasilimali
      • Serikali za Mitaa
      • Uhasibu na Fedha
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Sheria
      • TEHAMA
      • Afya
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Kitengo cha Habari na Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Morogoro
    • Mvomero
    • Gairo
    • Kilosa
    • Kilombero
    • Ulanga
    • Malinyi
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Morogoro
    • Morogoro DC
    • Mvomero
    • Gairo
    • Ulanga
    • Malinyi
    • Mlimba
    • Ifakara Mji
    • Kilosa
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uchimbaji wa Madini
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
    • Huduma za Ugavi
  • Machapisho
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
    • Fomu Mbalimbali
    • Ripoti mbalimbali
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Videos
    • Hotuba
    • Picha

SERIKALI YATUMIA TSH. 1.2 BIL. KURUDISHA MAWASILIANO MALINYI, RC MALIMA AMSHUKURU RAIS

Posted on: June 11th, 2024

Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  imetumia shilingi 1.2 Bil. kurejesha mawasiliano ya Barabara Wilayani Malinyi Mkoani Morogoro baada ya Mvua za Eli nino kuharibu miundo mbinu hiyo na kuacha mji huo ukiwa  kisiwani.

Hayo yamebainishwa Juni 11, 2024 na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima wakati wa ziara ya  Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa huo ambayo Mwenyekiti wake ni Mkuu wa Mkoa huo kwa lengo la kukagua miundombinu iliyoathirika na mvua za Elinino ndani ya Mkoa huo.

Akiwa Wilayani Malinyi, kiongozi huyo amewaeleza wananchi kuwa Mvua za Elinino zilileta uharibifu mkubwa wa miundombinu na kusababisha mto Furua kujaa maji na kumwaga katika mji wa Malinyi na kuvunja madaraja muhimu.

Hata hivyo, amesema baada ya uharibifu huo Waziri wa TAMISEMI Mhe. Mohamed Mchengerwa alifanya ziara Mkoani Morogoro, Pamoja na maeneo mengine alifika Wilayani Malinyi eneo lililoathirika na aliahidi kuleta fedha zitakazotumika kufanya matengenezo ya muda ya miundombinu hiyo wakati wanajipanga kwa ajili ya ujenzi wa kudumu.

Amesema, baada ya Waziri Mchengerwa kumwomba Dkt. Samia Suluhu Hassan fedha hizo na kuridhia, fedha hizo Shilingi 1.2 Bil. Tayari zilishaletwa na tayari zimefanya kazi ya kurejesha mawasiliano ndani ya Mji wa Malinyi.

Kwa sababu hiyo, Mhe. Adam Malima ametumia fursa hiyo kumshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuridhia fedha hizo za Matengenezo ya dharura kupelekwa Malinyi na kuwaletea wana malinyi mawasiliano yao huku akiwashukuru TANROADS kwa kazi kubwa waliyoifanya.

Naye Meneja wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) Mkoa wa Morogoro Eng. Alinanuswe Lameck Kyamba amesema Serikali imeleta fedha fedha zilizotengwa kwa ajili ya dharura na kazi ya kurejesha mawasiliano imefanyika ndani ya wiki mbili na sasa wanajipanga kwa ajili ya matengenezo ya kudumu.

Nao wananchi wa Mji wa Malinyi akiwemo Thobias Ndombaheka na Francis Gerlad kwa niaba ya wananchi wenzao wamemshukuru Rais Samia Suluhu kwa kuwafungulia tena mawasiliano yaliyokuwa yameathiriwa na Mvua na sasa wanaendelea na shughuli zao za kiuchumi bila usumbufu.

Barabara zilizofunguliwa ni pamojamna Barabara ya TARURA ya Malinyi – Igawa katika eneo la Kiwale Pamoja na Barabara ya TANROADS inayoingia Mjini Malinyi mbazo zote madaraja yake yalisombwa na maji ya mto Furua.


MWISHO


Matangazo

  • MATOKEO YA DARASA LA SABA 2024 October 30, 2024
  • View All

Habari Mpya

  • RC MALIMA AKEMEA ULANGUZI WA MAZAO.

    May 08, 2025
  • WAAJIRI MOROGORO WATAKIWA KUTATUA CHANGAMOTO ZA WAFANYA KAZI WAO.

    May 01, 2025
  • SERIKALI KUJENGA BARABARA YA LUPILO – MALINYI KWA KIWANGO CHA LAMI, Bil. 18 ZATOLEWA KUJENGA MADARAJA MAWILI.

    April 25, 2025
  • MWENGE WA UHURU 2025 WATAJA TUNU NNE ZA TAIFA.

    April 19, 2025
  • View All

Video

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima akikagua ujenzi wa jengo la ofisi mpya ya Mkuu wa Mkoa.
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Maelezo ya Mkoa
  • Tangazo la Zabuni
  • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
  • Hotuba
  • Taarifa kwa Umma

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Tanzania
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • TAMISEMI
  • Ikulu
  • Katibu Mkuu Kiongozi
  • Tovuti ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro

    Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO

    Simu: +2550232934305

    Simu: +255766828252

    Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.